MCHUNGAJI JOSEPHAT GWAJIMA AWACHAFULIA USEMI WATESI WA MAISHA YA WATU
Mchungaji Josephat Gwajima akionesha umahiri mkubwa katika upigaji wa Guitar. |
Ni wachungaji wachache wenye vipaya vingi kama alivyonavyo Mchungaji Josephat Gwajima |
Kila aliyekuwepo alimsifu Mungu Baba yetu wa mbinguni kwa hali ya kipekee sana. |
Kilikuwa kipindi cha sifa ambacho kilifanyika kuwa baraka sana |
Platform Choir wakisifu |
Mchungaji Yekonia Bihagaze akimkaribisha Mchungaji Josephat Gwajima |
Muimbaji wa Kimataifa wa Nyimbo za Injili Flora Mbasha |
SOMO:KUWACHAFULIA USEMI ADUI
Na. Mchungaji
Josephat Gwajima
Ufufuo na
Uzima,Tanganyika parkers Kawe
Utangulizi ZABURI
18
Mungu aliwaumba
watu na akawaagiza wazae na kuongezeka juu ya uso wa nchi lakini wakapatikana
watu waliokwenda kinyume na amri hiyo ya Mungu na kufanya kinyume, wao wakasema
watakaa mahali pamoja ili wasitawanyike usoni pa nchi. Unaanza kujifunza kumbe
wanaweza wakapatikana watu wakaenda kinyume na mambo yale ambayo Mungu amesema
juu ya maisha yako, Mungu anataka ubarikiwe, uwe na afya njema na ufanikiwe
lakini wapo waganga na wachawi na wanadamu ambao wanaweza kuja kinyume na
makusudi ya Mungu katika maisha yako.
Leo kwa jina la
Yesu tutawachafulia adui wote wa maisha yako usemi wao na utaanza kumuona Mungu
kwa namna ya ajabu tena katika maisha yako.
Mwanzo 1:27
Mungu
alipomuumba mtu alisema nendeni mkazae mkaongezeke mkaijaze nchi.
Mwanzo 11:1-7
“…Tushuke mpaka
huko tukawachafulie usemi…”
Baada ya kuwa
wameongezeka sana wakaamua kujenga mnara wa babeli ili wajikusanye mahala
pamoja wasije wakatawanyika katika nchi, wakapinganana agizo la Mungu. Mungu
baba, Mungu mwana na Mungu Roho mtakatifu wakaamua washuke duniani kuja kuwachafulia
usemi wasiendelee na makusudi yao ya kujenga mnara mpaka mbinguni.
Mungu alikuwa
ametoa amri ya awali kwamba enendeni mkaongezeke mkaijaze nchi, watu wakazaa wakaongezeka
kweli kweli, baadae akatokea kiongozi mmoja alietangaza kujenga mnara
utakaowakusanya mahali pamoja wasije wakatawanyika katika nchi. Nina wasiwasi
huyu bwana ndie aliekuwa mwanzilishi wa umoja wa mataifa wa wakati ule. Mungu
amesema tawanyikeni, halafu huyu bwana anasema wakusanyike mahala pamoja,
huwezi kupinganana agizo la Mungu na ukabaki salama.
Mungu amesema
ukaolewe wao wanasema hutaolewa, Mungu amesema muacheni huyu asome, wao wanasema
hasomi huyu, Mungu kasema mwacheni huyu akafanye biashara wao wanasema huwezi
fanya biashara, akazae huyu wao wanasema hata beba mimba, akafanye kazi huyu
wao wanasema hutafanya kazi, akamtumikie Mungu huyu wao wanasema huta mtumikia,
wanapingana na agizo la Mungu, leo tunawachafulia usemi wagombane wao kwa wao,
wasielewane wao kwa wao kamwe kwa jina la Yesu.
Unajua watu wakishakuwa
na lugha moja ni hatari sana, yaani wakiamua kunuia jambo ni lazima
watalifanikisha, kama wakiafikiana kwa lugha ya pamoja huyu bwana apate ajali,
yaani kikundi cha wachawi chote kikakubaliana apate ajali, kumbe tumegundua
wakiwa wanaongea lugha moja hawawezi kuzuiliwa neno, leo lazima tuwatengeneze,
tuwachafulie usemi wasielewane kabisa kwenye vikao vyao.
Kila maeneo kuna
vikundi vya wachawi na huwa wanakuwa na maeneo yao ambayo wanakusanyika usiku,
kwenye vikao vyao kuna mwenyekiti na wakikaa wanaanza kuleta hoja zao, tunataka
fulani avimbe tumbo, wakishakubaliana wanaongea lugha moja avimbe tumbo, mmoja
akisema avimbe mguu hapo lugha ishachafuka, hawatafanikiwa. Ila wakikubaliana
wote wataondoka kwa lugha moja kwenda kutekeleza adhma yao, kuwashinda hapo
mpaka mtu uwe unaishi sawasawa na sharia ya Mungu inavyotuagiza.
Joshua 8:12 “…akawaweka
kuotea kati ya Betheli na Ai…”
Wachawi huwa
wanaweza wakamuotea mtu hata kwa miaka mingi ili wafanye yale waliyoyakusudia
katika maisha ya mtu huyo, wakikubaliana kwa lugha moja ufe, watakufuatilia
mpaka wakushinde, wakifika wakikuta mtu huyu ameokoka yupo vizuri na Mungu,
wanaanza kukufuatilia ili siku ukamkosea Mungu ulinzi wa Mungu ukatoka kwako waweze
kufanikisha adhma yao. Namna ya kuwashinda hawa ni kuishi sawasawa na neno la
Bwana.
Hata ukija
serikalini kikundi cha viongozi wanao ongea lugha moja wakikubaliana jambo,
hawatazuiliwa na mtu. Kama CCM saivi wameanza kuongea lugha tofauti, hapo chama
ndio kinavyo meguka, maana Hawa wanasema Lowasa fisadi wengine wanasema huyu
msafi ndie mwenye uwezo wa kufanya maamuzi magumu. Kinachowaumiza CCM sasa ni
lugha tofauti, mnaemwita mwizi kwa wengine ni mzee wao, yule mnaemwita dhaifu
kwa wengine ni baba yao, na chama kilipo saivi kipo pabaya kweli kweli.
Hakuna kitu imara ambacho kikipewa lugha
tofauti kitaendelea kusimama. Mungu alivyoona wale watu wanaongea lugha moja na
wana mshikamano kweli kweli Mungu akaona awachafulie lugha na hawakufanikiwa
kuendelea na ujenzi wa mnara wao.
Ufufuo na uzima
pia tuna lugha yetu, na hakuna wakutuzuia, na ndio tunasambaa duniani hivyo kwa
lugha yetu hiyo moja. Tumeijaza Tanzania na sasa tunaelekea kuijaza dunia. Ili
jambo lifanikiwe lazima wawepo watu wanaoongea lugha moja, ukitaka kuwatawanya
wagawie lugha tofauti.
Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima akiwa anafundisha maelfu ya watu katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima |
Mchungaji Josephat Gwajima,Akihubiri nyuma yake wanaonekana na nyuso za furaha ni Mchungaji Bryson Lema(kushoto) na Mchungaji Baraka Tegge (kulia) |
Maelfu ya watu wa Mungu walikuwa wakiwekwa huru dhidi ya maadui zao wa kiroho |
Mtoto akiombewa na Mchungaji Josephat Gwajima |
Mchungaji Josephat Gwajima akipita katikati ya kundi la watu huku maombi yenye nguvu yakiendelea na watu wakiendelea kuwachafulia lugha maadaui zao. |
Kila jambo gumu
unalopitia usifikiri imekuja hivi hivi, kuna watu wanaongea lugha moja huko,
leo lazima tuwachafulie usemi. Leo walionitesa nakwenda kuwavisha kila mtu na
lugha yake. Kila aliefanya vita na wewe
nasema lugha tofauti zitaendelea kwenye vienge vyao kwa jina la Yesu. Na
adhma yao haitafanikiwa kwa jina la Yesu.
Makamanda watatu
wakishetani ni mpinga kristo,nabii wa uongo na Lucifer/shetani, leo
nikuwachafulia usemi hawa makamanda, muujiza wa kuwachafulia usemi unafanywa na
Mungu mwana, Mungu baba na Roho mtakatifu huwa wanashuka wenyewe kuchafua
usemi. Wanachafuliwa usemi wasielewane wao kwa wao, na wewe unasonga mbele na
Mungu na maisha yako
Hata mtu na
mkewe mkiongea lugha moja familia itajengeka, ila mkiongea lugha tofauti
mtatawanyika. Wawili hawawezi kwenda pamoja isipokuwa wamepatana, nami leo
nawachafulia usemi wawili waliopatana kukuangamiza hawatapatana kwa jina la
Yesu.
Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima |