http://www.mkcomputertweaks.com/mkgroup/fkbmksb.gifMatangazo

Tangaza nasi: mkatedaniel@gmail.com, +255 7666-00 69 70, +255 655-00 69 71, +255 787- 249594

Usilikose kila Jumapili

Jumanne, 29 Aprili 2014

REAL MADRID YAMALIZA UDHIA, BAYERN YALAMBWA 4-0

* Leo ni zamu ya Chelsea, Atletico Madrid

UNAWEZA usiamini ila ndivyo ilivyo, mabingwa watetezi wa Ligi ya Ulaya Bayern Munich wamevuliwa taji hilo baada ya kukandikwa mabao 4-0 na Real Madrid na kuwafanya wababe hao wa Hispania kutinga fainali.
Mpango wa kocha Carlo Ancelotti wa kuwapanga washambuliaji wake watatu Karim Benzema, Gareth Bale na Cristiano Ronaldo ulizaa mpango baada ya Real kuisambaratisha Bavarians nyumbani kwao bila kutarajiwa na kuzima ndoto za Pep Guardiola kubadilisha matokeo ya kipigo cha bao 1-0 ilichopewa timu yake katika  mechi ya kwanza.
Mabao mawili ya Sergio Ramos na mengine ya Cristiano Ronaldo yalitosha kukwamisha safari ya wababe hao wa Ujerumani kwenye uwanja wao wa Allianz Arena na kukubali kulitema taji hilo.
Ramos alianza kufunga bao la kwanza dakika ya 16 kwa pasi ya Luka Modric kabla ya kuongeza jingine dakika nne baadaye akimalizia pasi ya Pepe na Ronaldo alikuja kupigilia msumari katika dakika ya 34 kwa pasi ya Bale na kumalizia udhia dakika ya 90 kufunga bao la nne.
Real Madrid sasa inasubiri mshindi kati ya Chelsea ya England na Atletico Madrid wanaoumana leo katika mechi ya marudiano nyingine ya nusu fainali, mechi itakayochezwa mjini London.
Katika mechi ya kwanza timu hizo ziliotoka suluhu ya kutofungana na yeyeote eatakayetumia vyema karata yake ataifuata Real kwenye fainali ya Mei 24 mjini Lisbon Ureno.

Jumanne, 22 Aprili 2014

BREAKING NYUUUZ!!! HATIMAYE DAVID MOYES ATIMULIWA AKIWA MAZOEZI MAN UNITED



BAADA YA KIKAO CHA ASUBUHI: MAKAMU MWENYEKITI WA MAN United Ed Woodward AKIKABILIANA USO KWA USO NA KOCHA MOYES NA KUMUELEZA KUTIMULIWA KWAKE AKIWA MAZOEZINI ASUBUHI JUMANNE.

Jumamosi, 19 Aprili 2014

WASICHANA 14 ZAIDI WATOROKA BOKO HARAM

 19 Aprili, 2014 - Saa 04:11 GMT

vikosi vya Nigeria vyawasaka wasichana waliotekwa nyara

Kamishna wa elimu katika jimbo la Borno nchini Nigeria amesema kuwa wasichana 14 zaidi wamefanikiwa kutoroka katika mikono ya wanamgambo wa kiislamu waliowatekanyara Jumatatu usiku.
Musa Inuwo Kubo, amesema wasichana 44 sasa wamewatoroka watekaji hao na kwamba wasichana wengine 85 hawajulikani walipo.
Vikosi vya Usalama,makundi ya vijana wa kuweka usalama mitaani pamoja na familia za wasichana hao wanaendelea kuwatafuta.
Wasichana hao wanaaminika kutekwanyara na kundi la wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram.
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria amesema kuwa wasichana wamekuwa wakitekwanyara na kundi hilo lakini sio katika kiwango kama cha sasa.
Amesema kuwa wapiganaji hao wanapinga kuwepo kwa elimu ya kidunia na kwamba wanataka kuanzisha serikali ya kiislamu.

BBC

Urusi yaonywa kuhusu mkataba wa Ukraine


 19 Aprili, 2014 - Saa 06:42 GMT

Huku makubaliano yalioafikiwa siku ya alhamisi ya kupunguza hali ya wasiwasi nchini Ukraine yakikabiliwa na changamoto,waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry amewapigia simu maafisa wakuu katika serikali za Ukrain na Urusi.
Afisa mmoja wa wizara ya maswala ya kigeni nchini Marekani amesema kuwa bwana kerrry ameiagiza serikali ya Urusi kuafikia mkataba huo kikamilifu na mara moja.
Pia ameipongeza serikali ya Ukraine kwa hatua ilizochukua kuafikia mkataba huo.
Siku ya ijumaa wanaharakati wanaounga mkono Urusi walikataa kuondoka katika majengo wanayodhibiti mashariki mwa Ukraine,wakisisitiza kuwa uongozi mpya wa Ukraine ni sharti ujiuzulu kwanza.
Serikali ya mpito nchini Ukraine imetoa wito wa umoja wa kitaifa, ikiahidi kugatuwa mamlaka mbali na kuwahakikishia wakaazi wa eneo hilo la mashariki kwamba lugha ya kirusi itaendelea kuzungumzwa.

Ijumaa, 18 Aprili 2014

PAZIA LIGI KUU BARA LAFUNGWA, AZAM FC KUKABIDHIWA KOMBE CHAMAZI KESHO


Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inafikia tamati kesho (Aprili 19 mwaka huu) kwa timu zote 14 kuwa viwanjani, huku mabingwa wapya Azam wakikabidhiwa kombe lao Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam katika mechi yao dhidi ya JKT Ruvu.
Mechi zote saba zitachezwa kuanzia saa 10 kamili jioni ambapo Yanga na Simba zitakuwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa mechi ambayo viingilio vyake ni sh. 5,000 kwa viti vya bluu na kijani, sh. 10,000 viti vya rangi ya chungwa, sh. 20,000 kwa VIP C na B wakati VIP A itakuwa sh. 30,000.
Tayari tiketi zimeanza kuuzwa leo (Aprili 18 mwaka huu) katika vituo saba vya; Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Kariakoo (Kidongo Chekundu), Buguruni Shell, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Ohio na Samora, Ubungo OilCom, Dar Live Mbagala na Uwanja wa Taifa.
Mechi nyingine zitakuwa kati ya Tanzania Prisons na Ashanti United (Uwanja wa Jamhuri, Morogoro), Rhino Rangers na Ruvu Shooting (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora), Mbeya City na Mgambo Shooting (Uwanja wa Sokoine, Mbeya), Oljoro JKT na Mtibwa Sugar (Uwanja wa Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha) na Coastal Union na Kagera Sugar (Uwanja wa Mkwakwani, Tanga).