Rose Muhando ‘amkwaza’ Alex Msama
Rose Muhando- Muimbaji wa Injili
MUIMBAJI mahiri wa nyimbo za Injili
nchini na Afrika Mashariki, Rose Muhando, amemkwaza mkurugenzi wa
kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama, kwa kushindwa kuhudhuria Tamasha la Pasaka
katika mikoa ya Geita, Mwanza na Kahama mkoani Shinyanga.
Msama akizungumza na Kwetu Mbamba- bay, amesema kwa sasa hataki kufanya kazi na muimbaji huyo na hivyo kuamua kufuta mkataba naye.Amesema anashangazwa na tabia ya Rose kutokana na kumlipa kwa ajili ya tamasha hilo na pia kumtumia gari la kumfuata nyumbani kwake Dodoma, lakini ameshindwa kutokea.
Alex Msama- Mkurugenzi Msama Promotions
Hata hivyo, Muhando alipotafutwa ili kuelezea jinsi alivyomzingua Msama katika tamasha hilo, simu yake ya mkononi haikuwa hewani kwa muda mrefu.
Mwisho