http://www.mkcomputertweaks.com/mkgroup/fkbmksb.gifMatangazo

Tangaza nasi: mkatedaniel@gmail.com, +255 7666-00 69 70, +255 655-00 69 71, +255 787- 249594

Usilikose kila Jumapili

Jumatano, 23 Oktoba 2013

UVAMIZI KANISANI: MMOJA AUWAWA WAWILI WAJERUHIWA VIBAYA

UVAMIZI KANISANI: MMOJA AUWAWA WAWILI WAJERUHIWA VIBAYA..!


 
Wananchi wakiwa wakitafakari nje ya jengo la Kanisa la Gilgal Christian Centre lililopo Pasiansi Ilemela jijini Mwanza.
 ----------
Mtu mmoja ameuawa na wengine watatu kujeruhiwa kufuatia shambulizi lililofanywa na kundi la watu wasiofahamika usiku wa
kuamkia jana  katika kanisa la Gilgal Christian Worship Centre lililopo eneo la Pasiansi wilaya ya Ilemela jijini Mwanza.
Tukio hilo lililotokea majira ya saa saba usiku linamtaja Elia Lunyamila (35) ambaye ni mlinzi  na ni  mwenyekiti wa vijana wa kanisa kuuawa akiwa amejumuika kwenye ibada na waumini wengine Alex Msakuzi na Tumsifu Pungu ambao hali zao zinatajwa kuwa taabani wakipatiwa matibabu Hospitali ya Rufaa Bugando Mwanza baada ya kujeruhiwa vibaya kwa kukatwakatwa mapanga sehemu mbalimbali za miili  yao. 
Askofu wa kanisa hilo Eliabu Sentoz amelaani tukio hilo akilitaja kuwa ni la kinyama kwani limefanyika sehemu ya ibada akiwataka wananchi kuungana pamoja kulisaidia jeshi la polisi katika kutoa taarifa kuwabaini wahusika wa shambulio  hilo na akaiomba serikali kuongeza nguvu kukabiriana na wahalifu hao.
Kamanda wa polisi mkoa wa  Mwanza , Ernest Mangu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo mpaka sasa hakuna taarifa za kuibiwa kwa kitu chochote ndani ya kanisa, hali ambayo inalifanya tukio hilo kuwa na maswali mengi likihofiwa kufananishwa na yale ya uchomaji moto Makanisa.
Waumini wakitafakari tukio hilo la uvamizi lililosababisha taharuki kwa wakazi wa jiji la Mwanza.
 
 
Ndugu na majirani pamoja na waumini waliomfahamu marehemu Elia Lunyamila aliyeuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana wakiwa wamekusanyika nyumbani kwa marehemu kuomboleza
Askofu wa kanisa la Gilgal Christian Centre Eliabu Sentozi.
 
Chanzo: Masai Nyotambofu

SHAMBA LINAUZWA

SHAMBA LINAUZWA

LIPO KISANGA KISARAWE MBELE YA KIWANDA CHA SIMENTI.
UKUBWA NI EKARI MOJA KASORO KIDOGO.
BEI SH.MILIONI 6 (MAELEWANO YAPO)
LIPO JIRANI NA BARABARA LINA MAZAO MBALIMBALI
KAMA MAFENESI, MACHUNGWA, MACHENZA NA MITI YA MINAZI

WASILIANA KWA 0655 006971 AU 0755 006970
EMAIL: mkatedaniel@gmail.com

Jumatatu, 14 Oktoba 2013

KAMATI YA RUFANI YA MAADILI YA TFF YAFANYA MAPITIO

Msemaji wa TFF, Boniface Wambura

Kamati ya Rufani ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekutana jana (Oktoba 13 mwaka huu) kusikiliza maombi ya mapitio (revision) na mwongozo ya uamuzi wa Kamati ya Maadili.

Sekretarieti ya TFF iliwasilisha maombi ya mapitio kwa Kamati hiyo ya juu kabisa ya masuala ya maadili kutokana na ugumu wa utekelezaji wa uamuzi wa Kamati ya Maadili juu ya mashauri nane yaliyowasilishwa mbele yake.

Kamati ya Rufani ya Maadili itaendelea na kikao chake kesho (Oktoba 15 mwaka huu), na baadaye itakutana na waandishi wa habari (saa 10 jioni) kwa ajili ya kutangaza uamuzi wake juu ya mwongozo ulioombwa na Sekretarieti ya TFF.

KIONGOZI WA MWENGE AFUNGUA KITUO CHA IDYDCC
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Juma Ali Amir amefungua kituo cha kwanza cha Football for Hope kilicho mkoani Iringa kwa kuwataka wananchi kukituia vizuri ili wanufaike na huruma za kijamii zinazotolewa na taasisi ya IDYDC pamoja na kuendeleza mpira wa miguu.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kituo hicho jana (Oktoba 13 mwaka huu), kiongozi huyo amesema taasisi ya IDYDC (Iringa Development of Youth, Disabled and Child Care) wamefanya vizuri kuamua kutumia mpira wa miguu kusaidia jamii kwa kuelimisha juu ya mambo mbalimbali kama ugonjwa wa ukimwi, kusaidia walemavu, haki za watoto na afya ya jamii.
Naye Mwakilishi wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Patrick Onyango amesema amefurahishwa na kukamilika kwa kituo ambacho kitasaidia jamii.
Amesema idadi kubwa ya watu waliofika kwenye uzinduzi huo inadhihirisha ni kiasi gani kituo hicho kitakuwa na matokeo mazuri kwa jamii.
Onyango alisema hicho ni kituo cha 14 kukamilika kati ya 20 vinavyojengwa barani Afrika ikiwa ni mpango wa FIFA kurudisha kwa jamii mafanikio iliyopata kwenye fainali za kwanza za Kombe la Dunia barani Afrika.

Kituo hicho kina uwanja mdogo wa mita 20 kwa 40 uliowekwa nyasi bandia, jengo lenye ukumbi wa mikutano kwa ajili ya semina, chumba cha kupimia ukimwi, chumba cha ushauri nasaha, maktaba na ofisi.
Zaidi ya dola 270,000 za Marekani zimetumika kukamilisha ujenzi wa kituo hicho kilicho eneo la Mtwivila, Iringa mjini.

KESSY KUSIMAMIA MECHI YA KOMBE LA DUNIA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limemteua Mtanzania Lina Kessy kuwa kamishna wa mechi ya Kombe la Dunia Kanda ya Afrika kwa wanawake chini ya umri wa miaka 20 kati ya Botswana na Afrika Kusini.

Mechi hiyo ya kwanza ya raundi ya kwanza itachezwa nchini Botswana kati ya Oktoba 25 na 27 mwaka huu. Waamuzi kutoka Zimbabwe ndiyo watakaochezesha mechi hiyo namba tisa.

Waamuzi hao wataongozwa na Pamela Majo atakayepuliza filimbi wakati mwamuzi msaidizi namba moja ni Rudo Nhananga, namba mbili ni Stellah Ruvinga na mezani atakuwepo Tambudzi Tavengwa.

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Mashauzi kutambulisha mpya Idd el Hajj Da' West Tabata

Bendi ya taarabu ya Mashauzi Classic kesho itatambulisha nyimbo zao mpyakwenye onyesho maalum ya kusherehekea sikukuu ya Idd el Hajj katika ukumbi
wa Dar West Park, Tabata.
Onyesho hilo ambalo linajulikana kama 'Usiku wa Isha Mashauzi', imeandaliwa
na Keen Arts na  Bob Entertainment chini ya udhamini wa kinywaji cha
Konyagi, Straika, Kwetu Mbambabay  na Saluti5.
Isha
Mratibu wa onyesho hilo, Joseph Kapinga amesema kuwa onyesho litakuwa la
kipekee na maalum kwa kusherehekea sikukuu ya Idd El Hajj.
Amesema katika onyesho hilo, Mashauzi atatambulisha albamu yake mpya
ijulikanayo kama "Asiyekujua Hakuthamini" ambayo ina nyimbo kama "Mimi Bonge
la Bwana," utunzi wake Hashim Said, "Ropokeni Yanayoyahusu" ( Saida
Ramadhani) na "Haya ni Mapenzi Tu" (Zubeda Malik).
Zawadi mbalimabli zitatolewa kwa mashabiki wa bendi hiyo inayojulikana kama
Wakali wa Kujiachia.
"Tumeandaa zawadi mbalimbali kwa mashabiki wetu. Pia bendi ya Mashauzi
Classic watatumia onyesho hilo kutambulisha nyimbo zao mpya," Kapinga
alisema.
"Mashauzi Classic watapiga albamu zao zote. Matumaini yetu ni kuwa watu
watapata burudani ya kutosha kuliko siku zingine zote," alisema Kapinga.
Nyimbo zingine zitakazopigwa ni  "Viwavijeshi" (Issa Ramadhani), "Sitasahau
Yaliyonikuta" (Abdul Malik), "La Mungu Halima Mwamuzi" (Zubeda Malik) na
"Sijamuona Kati Yenu" (Rukia Juma).
Naye mkurugenzi wa bendi hiyo, Isha Mashauzi, alisema kuwa onyesho la Da
West litakuwa la kihistoria na kutaka watu wajitokeze kwa wingi ili historia
isiwapite.
"Kwa kweli bendi iko fiti," alisema Mashauzi.