Bendi ya taarabu ya Mashauzi Classic kesho itatambulisha nyimbo zao mpyakwenye onyesho maalum ya kusherehekea sikukuu ya Idd el Hajj katika ukumbi
wa Dar West Park, Tabata.
Onyesho hilo ambalo linajulikana kama 'Usiku wa Isha Mashauzi', imeandaliwa
na Keen Arts na Bob Entertainment chini ya udhamini wa kinywaji cha
Konyagi, Straika, Kwetu Mbambabay na Saluti5.
Isha
Mratibu wa onyesho hilo, Joseph Kapinga amesema kuwa onyesho litakuwa la
kipekee na maalum kwa kusherehekea sikukuu ya Idd El Hajj.
Amesema katika onyesho hilo, Mashauzi atatambulisha albamu yake mpya
ijulikanayo kama "Asiyekujua Hakuthamini" ambayo ina nyimbo kama "Mimi Bonge
la Bwana," utunzi wake Hashim Said, "Ropokeni Yanayoyahusu" ( Saida
Ramadhani) na "Haya ni Mapenzi Tu" (Zubeda Malik).
Zawadi mbalimabli zitatolewa kwa mashabiki wa bendi hiyo inayojulikana kama
Wakali wa Kujiachia.
"Tumeandaa zawadi mbalimbali kwa mashabiki wetu. Pia bendi ya Mashauzi
Classic watatumia onyesho hilo kutambulisha nyimbo zao mpya," Kapinga
alisema.
"Mashauzi Classic watapiga albamu zao zote. Matumaini yetu ni kuwa watu
watapata burudani ya kutosha kuliko siku zingine zote," alisema Kapinga.
Nyimbo zingine zitakazopigwa ni "Viwavijeshi" (Issa Ramadhani), "Sitasahau
Yaliyonikuta" (Abdul Malik), "La Mungu Halima Mwamuzi" (Zubeda Malik) na
"Sijamuona Kati Yenu" (Rukia Juma).
Naye mkurugenzi wa bendi hiyo, Isha Mashauzi, alisema kuwa onyesho la Da
West litakuwa la kihistoria na kutaka watu wajitokeze kwa wingi ili historia
isiwapite.
"Kwa kweli bendi iko fiti," alisema Mashauzi.