JUMAPILI AMBAYO UTUKUFU WA MUNGU ULIJIDHIHIRISHA KWA NGUVU KATIKA NYUMBA YA UFUFUO NA UZIMA KAWE-Dar es Salaam
PASTOR: SENIOR PASTOR
JOSEPHAT GWAJIMA
11th May 2014 , Sunday
Zaburi 27:1-14, Vita vya hali ni somo linaloendana na somo la matukio ya
kichawi
Ayubu1:19-24, Kuna vita vya
hali kwa mfano mtu anaweza kusikia uchungu, au hali ya hewa na mazingira kwa
mfano watoto wa Ayubu waliuawa na hali ya hewa ya upepo mkali . Ibilisi aliporuhusiwa
na Mungu kugusa maisha ya Ayubu na tukio mojawapo alilolitenda ni kuanza kuleta
hali mbalimbali ili kusudi watu wajue kuwa ni matukio ya hali ya hewa, shetani
alileta upepo tokea pande nne ukaipiga nyumba na watoto wa Ayubu wakafa. Rusifa
anasababisha hali ikiwa ni mojawapo ya silaha za kuwashambulia watu. Leo
tunataka tushindane na vita ya hali kwa jina la Yesu, Wanadamu wengi hawajui
kuwa shetani anatumia hali ya kushambulia maisha yao, kwa mfano hali ya moto,
mvua kali, upepo , hali ya mtu kujisikia Uchungu, hali ya kukosa amani nguvu
nakadhalika.
Leo tunatangaza kila silaha ya kukosa amani , kila
silaha ya woga na kila silaha ya hali itakayofanyika juu yako wewe
haitafanikiwa kwa jina la Yesu. Kwa
mfano tulipokuwa Ubungo kila siku nikitaka kuhubiri wingu linatanda na mvua
inanyesha na mimi mhubiri nalowana na
baada ya kugundua kuwa ni hali ya vita
kwa hiyo nikaanza kufunga anga kabla ya kuanza ibada.
Kuna matukio yanatangazwa kwenye vyombo vya habari kama
maafa ama majanga ambayo yametukia kutokana na hali mbalimbali lakini watu
wanapokea taarifa hizo bila kujua kuwa ni matukio ya kichawi yanayoletwa na
hali.
Kuna hali ya kuharibika biashara yako iliyotengenezwa,
hali ya kuachwa, hali ya kuumwa na hali mbalimbali zinazotengenezwa kinyume na
maisha ya mtu. Leo tunaenda kushindana kwa maana imeandikwa kwa maana
kushindana kwetu siyo juu ya damu na nyama bali juu ya falme mamlaka wakuu wa
giza na majeshi ya pepo wachafu. Je hayo mafuriko ni kawaida, siyo hiyo ni vita vya hali ya hewa ya mvua, maana
imeandikwa katika ufunuo “joka akafunua
mdomo na mto ukatoka ili kumgarikisha mtu, unaona joka alitoa mto , kumbe
shetani anaweza kutoa mto na kugharikisha watu.
Kwa hiyo mtu anaweza kutengenezewa hali ya hewa ya joto na akawasha AC
mpaka akachoka lakini joto liko palepale.
Kumbe shetani anaweza kunyoosha mkono wake na hali
fulani ikampata mtu, kwa mfano mtu anaweza kutengenezewa hali ya kutokutulia mpaka
ukimwuliza hawezi hata kuelezea hali yake.
Utaona shetani alitengeneza moto ukatoka mbinguni na kuteketeza kundi la
wanyama wa Ayubu.
Freemasons ni wakala wa shetani na wamepewa uwezo wa
kutengeneza hali mbalimbali juu ya mtu
kwa mfano wanakuwa na makongamano ya
kuzibadilisha fikra za watu hii ina maana wanatengeneza hali fulani ndani mtu ili
aamini kuwa mafanikio yanaweza kuja bila
uwezo wa Mungu. Watu wanaingizwa kwenye freemonson society kwa kuvutwa na
wenzao ,kwa kukaribishwa na kuambiwa maneno ya kutiwa moyo, kupewa zawadi na
kusaidiana kumbe huo ni mtego. Utasikia mtu anaambiwa kuwa kuna Society
inayoitwa Global Brotherhood inayosaidia watu kubadilisha mtazamo na fikra za
mtu kuelekea mafanikio makubwa. Hakuna kitu hapa duniani kinachoweza kutokea
chenyewe. Na duniani kuna makundi ya watu watatu:
I.
kundi la kwanza wasiojua
kinachoendelea na watu hawa ni kundi
kubwa na wanaweza kuitwa wapumbavu/ wajinga .
II.
kundi la pili ni wale wanaojua
kinachoendelea lakini hawajui jinsi ya kutenda kwenye hilo wanalojua.
III.
Kundi la tatu ni wale wanaojua
kinachoendelea na wanajua la kutenda kwenye hilo ninaloendelea hawa ni wachache
sana na wanaitwa wenye hekima/akili.
Uchawi una makundi matatu
·
Black magic – hawa ni wachawi
wanaoruka na kula nyama za watu na uchawi huu ufanyika kwa siri.
·
White magic -- uchawi
uliokubalika na jamii na ukitendwa watu wanaona hauna madhara mfano
wanamazingaombwe
·
Black Science - wanaweza
kutengeneza virusi vya magonjwa na
wakatupa kwa watu, wanaweza kutengeneza hali ya hewa fulani mfano matetemeko,
mvua kubwa nk.
Vifaa hizi vya hali ya hewa vinatengenezwa sehemu mbalimbali hata
wajapani wengi wanatengeneza vifaa hivyo. Hata kwenye biblia utaona Musa
alipoyapiga maji kwa fimbo yake ukatokea upepo mkali na bahari ikagawanyika ,
hiyo ulikuwa silaha ya hali. Leo
nakutangazia kwa jina la Yesu kuwa hakuna silaha ya hali ambayo itafanyika juu
yako na kufanikiwa kwa jina la Yesu.
Black science ni watu waliochukuliwa msukuleni na huko
wanakutana na mashetani na wanaanza kuwafundisha technologia ya kuonekana kwa
macho na hali ya hewa ni mojawapo ya
hizo technologia.kwa mfao Japani wametengeneza Train inayokwenda underground
kwa kasi sana 500km kwa saa na haina dereva inaendeshwa electronically , lakini
ukiwauliza mmetoa wapi hii technologia hawajui ilikotokea , lakini hii
inaonyesha kuwa mpinga Kristo analeta technologia hizi kuuleta ulimwengu pamoja
ili aweze kutawala vizuri wakati wake ukifika.
Hali mbalimbali zinaweza kutengenezwa kwa mfano ndege
kubwa yenye watu mia nne ikapotea kabisa , utajiuliza imekwenda wapi? Hii ni
hali imetengenezwa na ndege ikachukuliwa
na kuyeyushwa kabisa, hii inadhibitisha
kuwa ufalme wa giza unatenda kazi nyuma ya matukio. Nyakati hizi ni za kuwa
makini sana kwa maana shetani anatembea katikati ya watu na anajiungamanisha na
wanadamu. Kila mtu mchana wa leo aliyetengenezewa hali fulani kwa mfano hali ya
ugonjwa, hali ya umasikini, hali ya kukataliwa nk na mtu ametulia na kuridhika
leo nakutangazia kuwa Mungu anataka utoke kwenye hali hiyo kwa jina la Yesu. Kuna
watu wengine wametengenezewa hali ya kutojikubali , mtu anajisikia unyonge kila
wakati mpaka anaogopa kuwa kati kati ya watu wengine.
MAOMBI
Kwa jina la Yesu hali niliyowekewa ya kukataa ndoa, hali
ya kuogopa, hali ya kujikataa, hali ya kuwashwa naikataa kwa jina la Yesu, nami
leo navaa hali ya ujasiri na kuzishambulia hali za kishetani zinazonisumbua kwa jina la Yesu. Nawasha moto na kuteketeza
hali ya maumivu inayonisumbua, hali ya kukosa usingizi na hofu wakati wa usiku
, hali ya kujiona mnyonge na kujiona sifai, nayaamuru mapepo yanayohusika na
hali hizo yang’oke na kuniachia kwa jina
la Yesu.
Katika jina la Yesu kuanzia sasa nasimama kinyume na
hali yoyote ya kishetani iliyonipata, nasimama kinyume na silaha ya
hali iliyonipata kwa jina la Yesu. Nasambaratisha hali ya aibu iliyonipata,
hali ya kupata hasara kwenye biashara, hali ya ugonjwa na udhaifu kwa jina la
Yesu. Nakataa hali ya umasikini, hali ya unyonge, hali ya kuonewa, hali ya
magonjwa, hali ya aibu, hali ya kushindwa kwa jina la Yesu. Nawasambaratisha
mashetani wote wanaonifuatilia na kuniletea hali mbaya kwenye maisha yangu kwa
jina la Yesu. Imeandikwa kila silaha itakayofanyika juu yangu haitofanikiwa,
naamuru silaha zote za kuniletea hali mbaya zivunjike kwa jina la YESU. Imeandikwa
kila pando asilopanda baba yangu wa mbinguni litang’olewa, nang’oa hali ya
huzuni mliyonipandia, nang’oa hali ya uchungu mlionipandia kwa jina la Yesu.
Enyi mashetani mnaovaa sura za watu na sura za hali mbalimbali na kuja kunitesa leo nawaamuru kudhihirika na kutoweka kabisa kwenye maisha yangu kwa
jina la Yesu.
CHANZO: GCTC
**********************************AMEN************************************