Dk. Ashatu Kijaji...Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
http://www.mkcomputertweaks.com/mkgroup/fkbmksb.gifMatangazo
Tangaza nasi: mkatedaniel@gmail.com, +255 7666-00 69 70, +255 655-00 69 71, +255 787- 249594
Ijumaa, 20 Aprili 2018
DODOMA/SERIKALI
YAFAFANUA TRIL.1.5
Shughuli
za mkutano wa kumi na moja na kikao cha kumi na nne cha Bunge la Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania zimelazimika kusitishwa katika kipindi cha maswali na majibu
ili kuiwezesha serikali kutoa ufafanuzi kuhusu tuhuma za upotevu wa fedha
za serikali shilingi trilioni 1.5 ambazo kwenye taarifa ya mdhibiti na mkaguzi
mkuu wa hesabu za serikali CAG ilionyesha hazijulikani zimefanya matumizi gani.
Naibu
waziri wa fedha na mipango, Dk. Ashatu Kijaji, akitoa ufafanuzi bungeni mjini
Dodoma, amesema hakuna fedha za serikali ambazo zimezopotea wala kutumika
kinyume na matumizi yaliyoidhinishwa na bunge.
Amesema
fedha hizo ambazo taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ya
mwaka 2016/2017 iliyoishia june 30, mwaka jana na kuwasilishwa bungeni imeonyesha
serikali ilikusanya shilingi trilioni 25.3 lakini trilioni 23.8 ndizo
zilitolewa kwa ajili ya mishahara ya watumishi matumizi mengine matumizi ya
maendeleo na kulipa madeni yatokanayo na amana za serikali na riba na shilingi
trilioni 1.5 trilioni zilizobaki hazikujulikani zimeenda wapi.
Aidha
naibu waziri amefafanua zaidi kuwa matumizi ya fedha hizo yalikuwa bado
hayajahamishwa wakati ukaguzi wa CAG ukiendelea.
Fedha
ambazo zinadaiwa kupotea ni sawa na asilimia 6 ya fedha zote zilizokusanywa
kama mapato ya serikali kwa mwaka 2016/2017.
Mwisho
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)