http://www.mkcomputertweaks.com/mkgroup/fkbmksb.gifMatangazo

Tangaza nasi: mkatedaniel@gmail.com, +255 7666-00 69 70, +255 655-00 69 71, +255 787- 249594

Usilikose kila Jumapili

Ijumaa, 20 Aprili 2018


DODOMA/SERIKALI YAFAFANUA TRIL.1.5


Shughuli za mkutano wa kumi na moja na kikao cha kumi na nne cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimelazimika kusitishwa katika kipindi cha maswali na majibu ili kuiwezesha serikali kutoa ufafanuzi kuhusu tuhuma za upotevu wa fedha za serikali shilingi trilioni 1.5 ambazo kwenye taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG ilionyesha hazijulikani zimefanya matumizi gani.
Naibu waziri wa fedha na mipango, Dk. Ashatu Kijaji, akitoa ufafanuzi bungeni mjini Dodoma, amesema hakuna fedha za serikali ambazo zimezopotea wala kutumika kinyume na matumizi yaliyoidhinishwa na bunge.
Amesema fedha hizo ambazo taarifa ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ya mwaka 2016/2017 iliyoishia june 30, mwaka jana na kuwasilishwa bungeni imeonyesha serikali ilikusanya shilingi trilioni 25.3 lakini trilioni 23.8 ndizo zilitolewa kwa ajili ya mishahara ya watumishi matumizi mengine matumizi ya maendeleo na kulipa madeni yatokanayo na amana za serikali na riba na shilingi trilioni 1.5 trilioni zilizobaki hazikujulikani zimeenda wapi.
Aidha naibu waziri amefafanua zaidi kuwa matumizi ya fedha hizo yalikuwa bado hayajahamishwa wakati ukaguzi wa CAG ukiendelea.
Fedha ambazo zinadaiwa kupotea ni sawa na asilimia 6 ya fedha zote zilizokusanywa kama mapato ya serikali kwa mwaka 2016/2017.

Mwisho