SOMO: SHERIA MBILI ZA ROHONI
TAREHE: 19/10/2014
NA MCHUNGAJI KIONGOZI: JOSEPHAT GWAJIMA
Kuna ulimwengu wa roho na ulimwengu wa mwili. Mtu anapofanikiwa rohoni
baadae anafanikiwa mwilini. Inaweza kuwa magonjwa au ukawa na matatizo
yakikutokea mwilini jua kuwa yameanzia rohoni. Unapoanza kuomba na
kushambulia lazima utambue kuwa unashindana na ulimwengu wa
roho.Imeandikwa;
Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na
nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu
ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Waefeso 6:12
Kumbe kabla ya kubarikiwa lazima ubarikiwe rohoni. Tukizungumzia miji
ya kiroho, inamaana kwamba ulimwengu wa roho ni sawa na miji unayoiona
hapa duniani. Ukiona watu wanajua maneno au mistari ya biblia yote, sio
ishara ya kuwa yeye anauwezo wa kuyajua yote na namna ya kushindana.
Mungu ni roho, hivyo lazima tumwabudu katika roho. Imeandikwa.
Lakini Yesu hakujiaminisha kwao; kwa kuwa yeye aliwajua wote; Yohane2:24
Viumbe katika ulimwengu wa roho mfano, Mungu, malaika, mashetani
Viumbe wa kimwili ni kama wanadamu, kuku, simba, miti
Katika ulimwengu wa roho, kuna sheria mbili zinazouongoza. Mambo yote
huanzia katika ulimwengu wa roho, hasa katika ndoto. Zipo sheria 2,
zinazoongoza ulimwengu wa roho.
1. KUBADILIKA UMBO NA KUVAA UMBO LOLOTE
Ili mashetani ambao ni wachawi ili waweze kwenda kuroga lazima watoke
ndani ya miili yao na kuvaa umbo jingine. Kwa kuwa anakuwa rohoni
anaweza kuvaa umbo lolote, na kugeuka kuwa kitu chochote. Mfano, paka,
mbwa, kunguru. Lakini wachawi wanaposikia hukutambua kuwa ni wachawi
wanafurahi sana. Imeandikwa; Marko 16:12
12 Baada ya hayo akawatokea watu wawili miongoni mwao, ana sura nyingine; nao walikuwa wakishika njia kwenda shamba.
Yesu aliwatokea wanafunzi wake akiwa na sura nyingine, lakini kwa kuwa
alikuwa rohoni, alionekana kuwa na sura nyingine. Yesu anasura nyingine,
kama umezoea kumuona daktari leo anasura nyingine, akitaka kukutokea
kama mmea natakutokea kama ua la sharoni, au mzee wa siku, lazima
utambue kuwa laizima atokee kwa sura nyingine.
Ukiri; leo katika
jina la yesu yesu akutokee kwa sura nyingine, kama umezoa yesu ni
mponyaji tu leo anasura nyingine, ni mfariji, ni mfalme wa wafalme, ni
mwamba wa kale. Leo lazima yesu atokee kwa sura nyingine sawa na tatizo
ulilonalo. Amen.
Yesu aliamua kubadili sura lakini wanafunzi wake
walijua ni yeye. Kila unapoongezeka kila hatua unaongeza marafi
unaongeza maadui pia. Lakini kama ulikuwa umezoea kutembea kama chura
tambua kuwa unatakiwa kuruka juu kama tai. Imeandikwa;…………………………….
Yohana20;15
15 Yesu akamwambia, Mama, unalilia nini? Unamtafuta
nani? Naye, huku akidhania ya kuwa ni mtunza bustani, akamwambia, Bwana,
ikiwa umemchukua wewe, uniambie ulipomweka, nami nitamwondoa.
Nirahisi sana watu kukuamini lakini mtu aliyekuzoea hawezi kukuamini
kirahisi, ndiyo maana Yesu alimtokea mama yake kwa sura nyingine kama
mtunza bustani, ili aweze kumwamini. Watu wamemzoea yesu wa kuponya
magonjwa tu lakini yesu anatokea kwa sura nyingine ili mambo yaweze
kutokea na kumwamini.
Hivyo ili uweze kufanya ya rohoni lazima uvae sura nyingine. Imeandikwa; ufunuo 1:9
9 Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika
mateso na ufalme na subira ya Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa
kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu.
10 Nalikuwa katika Roho, siku ya Bwana; nikasikia sauti kuu nyuma yangu, kama sauti ya baragumu,
Roho inaweza kuvaa sura yoyote ndiyo maana Yesu alimtokea Yohane katika sura nyingine kwenye kisiwa cha Patmo.. Imeandikwa;
Bwana akamtokea Ibrahimu karibu na mialoni ya Mamre, alipokuwa ameketi
mlangoni pa hema yake mchana wakati wa hari. Akainua macho yake akaona,
na tazama, watu watatu wamesimama mbele yake. Naye alipowaona alipiga
mbio kuwalaki kutoka mlangoni pa hema, akainama mpaka nchi, Mwanzo18;
1-2
Kumbe roho inaweza kugeuka na kuwa kitu chochote, na kufanaya kazi kama wanadamu. Imeandikwa;
Huwafanya malaika zake kuwa pepo, Na watumishi wake kuwa moto wa miali. zaburi 104:4
Ukishaona matukio kama hayo unahisi ni upepo kumbe kuna watu ndani ya
upepo. Unaweza kuona upepo unakuja ukahisi ni upepo kumbe ni mjomba au
bibi yuko ndani ya upepo. Lazima utambue kuwa kuna upepo unaosumbua
hali ya maisha yako ndo maana unaona taabu na misukosuko.
Yesu
alisema na tuvuke ng’ambo ya pili lakini shetani aliyajua hayo na
kutikisa chombo. Tambua hata wewe kwenye maisha yako ukiona umepanga
kufanya jambo lolote la maendeleo na mara gafla matatizo yanaanza
usikubali pigana maana ni upepo huo umetengenezwa ili usifike unakoenda
au usifanye unachotaka kufanya. Imeandikwa;
Ndipo Farao naye akawaita wenye akili na wachawi; na hao waganga wa Misri wakafanya vivyo kwa uganga wao.
12 Wakabwaga chini kila mtu fimbo yake, nazo zikawa nyoka; lakini fimbo ya Haruni ikazimeza fimbo zao. Kutoka 7; 11-12
UKIRI
Kuanzia leo kila atakae jigeuza kwa sura yoyote nitamuona kwa Jina la Yesu.
Haimanishi kuwa mashetani wanaouwezo wa kutengeneza chura, au nyoka au
fimbo ila tu waliweza kunuizia kitu kikageuka na kutimiza lengo. Malaika
anaweza kufanya vile hata mashetani wanaweza kuvaa sura na maumbo ya
kitu na kutimiza kusudi. Imeandikwa;
Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru.2Wakoritho 11:14
AINA NNE ZA MASHETANI
1. Majoka amabao ni roho ya uovu walioanguka kutoka mbinguni baada ya
uasi. Kulikuwa na vita mbinguni; Mikaeli na malaika zake wakapigana na
yule joka, yule joka naye akapigana nao pamoja na malaika zake; Ufunuo
12;7
2. Mizimu. Haya ni mashetani waliotawala ukoo kwa muda mrefu.
3. Miungu. Ni mashetani waliopewa makafara kwa muda mrefu na wakapewa nguvu na kuwa miungu
4. Majini. Hawa nai mashetani wenye asili ya kiarabu.
Imeandikwa;
Nikaona roho tatu za uchafu zilizofanana na vyura, zikitoka katika
kinywa cha yule joka, na katika kinywa cha yule mnyama, na katika kinywa
cha yule nabii wa uongo. Ufunuo 16:13
Akalia kwa sauti kuu,
akisema, Umeanguka, umeanguka Babeli ule mkuu; umekuwa maskani ya
mashetani, na ngome ya kila roho mchafu, na ngome ya kila ndege mchafu
mwenye kuchukiza; Ufunuo 18:2
Nguvu kubwa ya mashetani ni ule
uwezo wa kutowatambua. Wanapotoka ndani huwa wananuiza na kuvaa maumbo
bandia. Wachawi nao huwa wanasikiliza kama umewatambua, wakiona umeona
visivyo wanafurahi maana wanajua kuna biashara inaendelea na
wamefanikiwa.
Ukiri.
Kuanzia leo lazima kila atakekuja kuniroga
nitamuona kwa jina la Yesu.Kila aliyegeuza umbo naamuru nimuone katika
umbo lake la siri.
Watu wengine wanajisikia kama wana misumari ndani
ya miili yao lakini jambo amabalo hukulijua kama limetengenezwa an
kugeuka kuwa kisu ndani ya miili yao. Ukiona nchi inayumbayumba lazima
ujue kuna chanzo chake kiko katika ulimwengu wa roho. Ukishinda rohoni
unaweza kuua kwa siraha isiyorasmi .
Yawezekana umeumwa sana na hujui namna ya kutatua tatizo ulilonalo.Imeandikwa;
Inawezekana, unajisikia hali mbaya hasa ya kumtukana mume wako, au mke
wako lakini kwa akili zako huwezi kusema vile, lakini ukajikuta unasema
vile. Kimsingi kuna viumbe wa rohoni wanakaa ndani yako ndo maana
wakati mwingine unajikuta umeshatukana.
Inawezekana, unaona uso wako
unaweka makeup, lakini sura iko kama babu, jambo usilolijua ni kuwa
yuko aliyetumwa na kugeuka na kuwa babu.
MAOMBI
jini, joka,
mzimu, aliyegeuka umbo na kuja kwangu, lazima nikuone katika jina la
yesu.nina waamuru wapigwe katiak jina la yesu.Mimi ni askari naangusha
ngome za balaa, ngome za mikosi, ngome za magonjwa katika jina la Yesu.
Mimi nakataa kutawaliwa katika jina la yesu.
Kuanzia sasa roho
yoyote iliyogeuka na kuwa balaa, talaka, mikosi, magonjwa, naivunja
katika jina la yesu. Kwa jina la yesu kuanzia leo chochote kilichotumwa,
nilichikinunua, nakiangamiza katika jin layesu. Kitu chochote, au roho
yoyote, iliyondani ya nyumba yangu naivunja, na irudisha ilikotoka
katika jina la Yesu.
Kwa jina la yesu,
2. UNAMFUMBA MTU ASIKUTAMBUE.
Katika sheria mbili za rohoni pili ni kukufumba usimtambue, na wewe
ukiona unahisi ni vitu hivyo ulivyoviona kwa macho au katika ndoto.
Akili ya mtu akifungwa mtu akiona hatambui kama ni wachawi au mashetani.
Yawezeka kila ukilala na kuota ndoto ukiamka unaanza kusema uliyoyaota
ambayo yako katika sura bandia. Inatakiwa uwafunge ili wasijifiche
wakija uwatambuae katika jina la Yesu. Omba maombi haya kwa jina la
Yesu. Maana imeandikwa Imeandikwa ;
Nanyi mkiomba lo lote kwa jina
langu, hilo nitalifanya, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana. Mkiniomba
neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya Yohana 14:13-14
MAOMBI
Katika jina la yesu namteketeza mtu yeyote aliyejigeuza sura ili anitese namfyeka katika jina la yesu.
Kila atakaekuja katika umbo lolote lazima nimjue katika jina la Yesu,
ninawafunga wasinitambue kama nimewaona. Kuanzia leo naamka toka
usingizi wa kiroho, na akili yangu iwaze kutawala, iwaze biashara katika
jina la Yesu . Kuanzia leo naanza kutambua kazi yangu, nianze kuelewa
kazi ya kufanya, biashara ya kufanya, katika jina la Yesu.
Nawashambulia mashetani wote katika jina la Yesu, mashetani
walioshikiria familia yangu, kazi yangu, ndoa yangu, biashara yangu
katika jina la Yesu nawaangamiza katika jina la Yesu. Nawaangamiza
maadui wote katika jina la Yes. Natumia mamlaka aliyonipa Yesu nawafyeka
wanaozuia kazi yangu nawafyeka wanaozuia ndoa yangu, nawafyeka
wanaozuia huduma yangu, katika jina la Yesu. Nawashambulia kwa damu ya
mwanakondoo.
Imeandikwa;
Kila silaha itakayofanyika juu yako
haitafanikiwa na kila ulimi utakaoinuka juu yako katika hukumu
utauhukumu kuwa mkosa. Huu ndio urithi wa watumishi wa Bwana, na haki
yao inayotoka kwangu mimi, asema Bwana. Isaya 54:17
Nawafyeka
katika jina la Yesu, mtu yeyote aliyesimama kwenye njia zangu kunizuia
nisifanikiwe, kuzuia nisisonge mbele kunizuia nisipate ajira, nafunga
uwezo wako wa kujigeuza na kuwa balaa, nakujigeuza kuwa mikosi, kuwa
matatizo ,kuwa mtego na balaa, nawashambulia katika jina la Yesu.
Naharibu uwezo wenu katika jina la Yesu, ng’oa madhabahu zenu katika
jina la Yesu. Nawatiisha, na kata mamlaka zenu, kaila kiumbe
kinachotumia mazira kuharibu maisha yangu nawashambulia katila jina la
Yesu. Naaribu uweza wenu wote katika jina la Yesu.
Natangua yote
uliyoyapanga katika jina la Yesu. Imeandikwa; yeye uyatangua mashauri ya
wadanganyifu na mikono yao isipate kutimiza makusudi yao.
Kila
vibarua wa shetani mnaovaa sura bandia nawaangamiza katika jina la Yesu,
navunja kila laana ya familia iliyonipata kupitia viumbe wa rohoni
mnaojibadilisha sura na kuniroga nawafyeka katika jina la Yesu.
Kila
nguvu ya giza inayotawala nailaani katika jina la Yesu, kila balaa
zinazotawala nazivunja katika jina la Yesu. Nakiri leo niko huru, kazi
yangu iko huru katiaka jina la Yesu. AMEN
Inua mikono juu; na ukiri maneno haya kwa nguvu
Kila jini aliye ndani yangu uliyeingia ili mimi nisiolewe, ili
uniletee balaa, imeandikwa lolote mtakalolifunga hapa duniani ,
litafungwa na mbinguni ewe jini uliyetumwa ofisini kutoka kijijini,
nakuapisha dhihirika na ujulikane kwa jina la Yesu. Jini makata, jini
wa hasira, jini wa mikosi, kila aliyerogwa kwa kuwekewa dawa kwenye
tumbo la uzazi, kwenye maji ya kuoga, kwenye chakula, kwenye kitanda,
kwenye nguo, kwenye damu wakati wa siku zangu naamuru moto ndani yangu
ukuunguze na unitoke katika jina la Yesu.
-----------------------------------AMEN---------------------------------------------