http://www.mkcomputertweaks.com/mkgroup/fkbmksb.gifMatangazo

Tangaza nasi: mkatedaniel@gmail.com, +255 7666-00 69 70, +255 655-00 69 71, +255 787- 249594

Usilikose kila Jumapili

Ijumaa, 24 Januari 2014

YANGA UTURUKI WATUA DAR

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom nchini Tanzania Bara, Yanga wamewasili salama jijini Dar es salaam wakitokea jijini Antalya nchini Uturuki walipokuwa wameweka kambi ya wiki mbili kwa ajili ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu na mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Young Africans imetua uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl JK Nyeree majira ya saa 9:30 alfajiri kwa shirika la ndege la Turkish Airline na moja kwa moja kikosi cha wachezaji 27 na benchi la Ufundi kimeingia kambini kujiandaa na mchezo huo wa kesho.
Kocha mkuu wa Young Africans Hans Van Der Plyum amesema anashukuru kikosi chake kimefika salama jijini Dar es salaam na amesema vijana wake watafanya mazoezi mepesi leo jioni kabla ya kesho kushuka dimba la Uwanja wa Taifa.
Akiongelea kambi ya Antalya Hans amesema kambi ilikuwa nzuri na mafanikio makubwa kwani vijana wameonyesha uwezo wa hali ya juu katika nidhamu, kujituma, upendo na kushirikiana kitu ambacho ndio nguzo ya timu kufanya vizuri.
Aidha Hans amewaomba wanachama wa Young Africans, wapenzi na washabiki kesho kujitokeza kwa wingi kuja kuishuhudia timu yao iliyokuwa kambini Uturuki itakapocheza na wauza mitumba wa Ilala Ashanti United na kuitambulisha staili yao ya uchezaji kutoka Antalya.

Jumatatu, 13 Januari 2014

IBADA YA JUMAPILI KANISA LA UFUFUO NA UZIMA- KAWE

MAELFU YA WATU WA MUNGU WAANZA MAISHA MAPYA KATIKA IBADA YA JUMAPILI NA MCHUNGAJI JOSPHAT GWAJIMA

Ibada ya Jumapili ya Tarehe 12.01.2014 katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima Kawe yawa ya Manufaa makubwa sana kwa Maelfu ya watu waliofika Ibadani, ni Baada ya Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima kutangaza rasmi kuwa ni siku ya, kufanya maombi na watu kujiweka huru dhidi ya matatizo na laana za familia.



SOMO: MATATIZO YA FAMILIA/UKOO
Na. Mch Josephat Gwajima
1 Mambo ya Nyakati 1:1-54
Ni kitabu cha kushangaza sana kwenye biblia sababu kinaelezea tu Fulani akamzaa Fulani, ni kitabu kilichokuwa inanipa taabu sana kukisoma kwenye biblia sababu majina mengine ni magumu hata kuyatamka, nikawa najiuliza hiki kitabu kinamaanisha nini na kwanini kimeandikwa kwenye biblia, nilikuwa sielewi ni nini mtu unaweza kujifunza kwa kuambiwa huyu akamzaa huyu.
Niliposoma kwenye 2 Timotheo 3:16 nikaona kila andiko lililoandikwa lafaa kwa mafundisho, nikajiuliza sasa haya majina ya watu kwenye hiki kitabu yanatufundisha nini? Nilipokuwa natafakari kitabu cha mambo ya nyakati nikapata shock (mshtuko) baada ya kusoma Mathayo 1:1-17 nikaona kitabu hiki kimeanza kwa kuandikwa hiki ni kitabu cha ukoo wa Bwana yesu, nikajiuliza hee hivi Yesu tena ana ukoo.

Nilipoanza kufuatilia huyu Mungu anataja ukoo tena kwanini, 2 Wakorintho 5:17 hata imekuwa mtu akiwa ndani ya kristo amekuwa kiumbe kipya, sasa haya mambo ya ukoo nini tena, niliposhuka kidogo nikaona haya ndiyo makabila 12 ya Yakobo, nikashangaa zaidi kumbe Mungu anajishughulisha na makabila tena. Hapo ndipo nikaanza kujifunza maisha ya mtu anayoishi leo, kama hauishi maisha yanayo mpendeza Mungu maisha yako yatakuwa sawasawa na kabila au ukoo anaotoka. Nikagundua kumbe kuelezea mambo ya familia hakuna tatizo maana hata Mungu yeye mwenyewe ameelezea sana kwenye biblia.


Nikaanza kufuatilia baadhi ya familia nikaona hata usome vipi huwezi kupata upenyo wa maisha, hata Mungu akikuinua kukupeleka ulaya litatokea jambo Fulani litasababisha urudi tu sababu familia hii hawaruhusiwi kupenya, familia hawaruhusiwi kutajirika, familia hawaruhusiwi kumuriki nyumba, familia hawatakiwi kumiriki magari.
Unaweza kuwa umeokoka, lakini kama hujadili na haya mambo ya familia utaingia mbinguni ukiwa umechoka, umekung’utwa kwelikweli, umeokoka lakini unaishi maisha magumu kweli,  unajiuliza mbona kwenye Mathayo 11:28 imeandikwa njooni kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo nami nitakupumzisha, unashangaa mbona mimi sipumziki, kumbe unatoka ukoo wa taabu wenye kulemewa na mizigo na laana (huo ni ukoo wa kutokupumzika).



Hebu jaribu kuangalia maisha ya baba yako na namna alivyo/anavyo malizia maisha yake, kama hakuna jitihada za ziada na wewe utamalizia maisha vile vile. Yesu alikuja ili tukatae kuwa na maisha kama waliyonayo baba/babu zetu, wewe umemuamini Yesu ili akuondolee yale maisha aliyoishi baba yako. Usiseme ukoo wetu sio ukoo wa viongozi, ukoo wetu hatufanikiwagi, ukoo wetu wanakufaga na umri mdogo, usiseme maneno hayo. Useme mama yangu alimaliza hivi lakini mimi nasimama na Bwana Yesu naamua kwenda beyond average, naamua kwenda mbele Zaidi. Usifuate kawaida wewe ukishakuwa umeokoka hauendi kwa kawaida za binadamu.
Ndio maana tunavoanza kuomba tunasema Mungu wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo hapa tunakuwa tunajiungamanisha na utajiri na Baraka zote za Ibrahimu, Isaka na Yakobo. Kabla ya Ibrahimu kulikuwepo na kina Serugi, Tera na kina Nahori lakini hatuanzii huko maana Serugi alikuwa na matatizo yake, Ibrahimu alitengwa na jamaa zake akaambiwa aende kwenye nchi atakayokabidhiwa. Wokovu ni kutengwa, kutengwa na taratibu za ndugu, jamaa, umasikini na mabalaa ya familia. Hivyo ukishaokoka tu maana umetengwa, hupaswi kuwa kama alivyokuwa mama yako au baba yako au babu yako uende extra mile na pale walipoishia walipokutangulia.
 
Sababu itakayokufanya ukimbie kwa nguvu zote kwenda mahala pengine
Mwanzo 9:18-26
“…Hamu ndiye baba wa kanaani…”, “…Hamu baba wa kanaani akauona uchi wa baba yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje…”
Ukisoma hayo maandiko utaona Hamu amefanya kosa na baba yake akamlaani kanaani na kizazi chake, na ukiendelea kusoma biblia utaona hiyo laana inavyozidi fuatilia kizazi cha kanaani. Kumbe hata leo kuna matatizo ambayo mtu unaweza kuwa nayo, sio kwamba yamesababishwa na maisha yako unayoishi leo hapana, bali yamesababishwa na makosa waliyo fanya babu wa ukoo, hiyo laana waliyolaaniwa ndiyo inayoendelea kukutafuna hii leo.
Nuhu akalevuka kutoka katika ulevi wake akamlaani kanaani, kanaani analaaniwa kwa kosa la baba yake, aliyeona uchi wa baba ni Hamu lakini laana ikamuangukia kanaani ambaye ni motto wa Hamu. Hapa tunajifunza kile kilichofanyika na mababu kina sambaa kwenye ukoo na vizazi vyote vijavyo, kama ni laana itasambaa kwenye kizazi chote, kama ni Baraka itasambaa kwenye kwenye vizazi na vizazi.
Hebu tuangalie maisha ya watoto waliozaliwa na kanaani
Mwanzo 10:15-19
Ukisoma hapo utaona kabila za wakaanani zikatawanyika na hata sodoma na gomora ilitokea hapo kwenye ukoo wa kanaani, unajiuliza hawa watu wa sodoma na gomora kwanini wanatenda uovu huu, kumbe ni laana ambayo imeendelea kuwafuatilia, hata kuteketea.
Kutoka 3:17
Mungu anasema atawapandisha watu wake kutoka katika mateso ya misri na kuwaingiza katika nchi ya mkaanani nchi iliyojaa asali na maziwa. Utagundua hapo, hawa wakaanani wananyang’anywa nchi yao na watu wa Mungu.
Kutoka 23:23 atawakatilia mbali wa Yebusi, unajiuliza hawa watu wamekosa nini mpaka wapate mateso yote haya, tunagundua ni lile kosa la Hamu kuona uchi wa baba yake, kosa hawakufanya hawa ukoo wa Kanaani lakini ndio laana inaendelea kuwafuatilia.
Kutoka 33:2 “…Nitawafukuza…” Kumbe kufukuzwa ni dalili ya laana
Kumb 20:17
Lakini uwaangamize kabisa Mhiti, na Mwamori, na Mkaanani, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi kama alivyokuamuru Bwana Mungu wako. Utaona hapa laana inawafanya hawa watu waangamizwe kabisa, wengine hata hawajui kulikuwa na Hamu ambaye alitenda kosa, lakini laana inaenda nao, na kamwe haiwaachi. Nawe ndivyo ilivyo kuna laana inakufuatilia ambayo leo lazima tuifanyie kazi.
1 Petro 1:18 “…Mwenendo wenu usiofaa mliupokea kutoka kwa baba zenu…” Kumbe kuna mambo yasiyofaa yanayowapata watu leo yalitoka kwa baba zao.
Mambo yaliyokupata kwenye maisha yasikuzuie kupaa kwenda kwenye kesho yako, yote yaliyokupata yalikuwa ni kukunoa uwe upanga mkali kwa ajili ya kesho yako.
Inawezekana leo una laana sababu ya makosa waliyofanya babu zako, babu yako alitesa wenye haki, babu yako alifanya mauaji akalaaniwa na laana inaendelea kwako hadi leo, leo ujitenge na laana za familia, Ibrahimu alitengwa na jamaa na ndugu zake akatangaziwa Baraka na kizazi chake chote hata kuzaliwa kwa Bwana Yesu.
Tanzania maeneo ambayo Mungu asiye Yehova alipoabudiwa kwa muda mrefu ndio masikini kuliko maeneo yote, hiyo ni kwa sababu ya laana ya kuabudu miungu mingine “Biblia inasema usimuabudu Mungu mwingine ila mimi Zaburi 81:9” laana hiyo inakufanya uwe replaced Mungu anakutoa na kumpa mwingine. Unapomuabudu Mungu mwingine ambaye sio Yesu unashangaa watoto wako wanaanza kuondolewa, watoto wako wanaondolewa ni laana hiyo, wakati mwingine unaamua wewe mwenyewe kuacha wenzako wanamiriki.


Namna nzuri ya kutoka kwenye ukoo ni kutoka kama alivyofanya Ibrahimu akaambiwa toka leo kwa jamaa na ndugu zako nenda mpaka nchi nitakayokuonyesha. Kutoka kwetu leo kwenye familia sio kukataa familia, tunatoka kwa namna ya rohoni, tunajitenga na laana zote za familia, unapofanya hivyo mashetani waliotawala familia yako kwa muda mrefu wanakosa nguvu ya kukufuatilia.
Kila unapokataa kwenye ulimwengu wa roho unavunja kitu, unabomoa kitu, na mashetani waliotumwa kulinda ukoo wanakimbia wanajua huyu mtu katukataa.
 
Leo ukatae na kuhama kwenye ukoo wa laana, ukoo wa umasikini, ukoo wa balaa, uhamie ukoo wa Ibrahimu, Isaka na Yakobo, ukoo wa Bwana Yesu. Jitenge na mikosi yote, umasikini kwa jina la Yesu. Ufanye hivyo kwa kumaanisha, na hakika yake utabadirika, hutakuwa kama ulivyo kwa jina la Yesu.

SOMA HABARI HII: 'Niliula mguu wa adui kulipiza kisasi' CAR


 
Huku hali ya taharuki ikiendelea kutanda kati ya jamii za waisilamu na wakristo katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, BBC imegundua mambo ya kutisha yanayofanyika mjini Bangui, mji mkuu wa taifa hilo.
Wanaoyashuhudia baadhi ya mambo hayo wameambia BBC kuhusu kisa cha mwanamume mmoja anayejulikana kwa jina la utani kama "Mad Dog," kuwa alimkata mguu muisilamu mmoja baada ya kumuua akisaidiwa na umati wa watu na kuula.
Mwanamume aliyekifanya kitendo hicho ameambia BBC kuwa alifanya hivyo kama hatua ya kulipiza kisasi baada ya wapiganaji wa kiisilam kumuua mkewe aliyekuwa mja mzito na wifi yake pamoja na mwanawe.
Aidha mwanamume huyo kwa jina Ouandja Magloire alisema kuwa kila mtu ameghadbishwa na wapiganaji waisilamu na hakuna atakayewasamehe kwa walichokifanya.
Anasema alimuona mwathiriwa akiwa ameketi ndani ya basi moja. Alimtoa nje na kuanza kumshambulia na punde si punde akasaidiwa na umati uliokuwa unashuhudia kitendo hicho ambao pia ulimshambulia mwathiriwa huyo.

"Muisilamu! Muisilamu! Muisilamu!. Nilimdunga kisu kichwani na kummwagia petroli kisha kumteketeza. Baadaye nikaanza kuula mguu wake mmoja kwa Mkate hadi kwenye mfupa. Ndio maana watu wananiita Mad-dog," alisema Magloire.

'Nilifanya hivyo kwa sababu nina uchungu mwingi, wala sina sababu nyingine.''
Hali ilivyo kwa sasa katika taifa hilo hakuna hata mtu mmoja aliyejaribu kumnusuru mwathiriwa. Jamhuri ya Afrika ya Kati imekumbwa na ghasia za kidini tangu Disemba mwaka jana ambapo wapiganaji wa kiisilamu walimsaidia aliyekuwa Rais michel Djotodia kuingia mamlakani kwa njia ya mapinduzi.
Kisa hiki hata hivyo kimewashangaza wengi sana . Na hali hii ikijiri, Mamia ya wanajeshi wa serikali walioasi jeshi na kujiunga na wapiganaji wakristo katika vita vyao dhidi ya waisilamu,wameanza kurejea katika kambi zao za kijeshi.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, wanajeshi hao wengi wao wakiwa wamevalia mavazi ya kiraia walitia saini makubaliano na wakuu wa jeshi kabla ya kurejea kambini. Ni kutokana na ombi la mkuu wa majeshi Ferdinand Bomboyeke, aliyewasihi kurejea kambini Jumatatu.

Source: BBC

Jumatatu, 6 Januari 2014

Bashir kukutana na Salva Kiir

Bashir anakutana na Kiir kwa mara ya kwanza tangu vita kuanza Disemba 15
Rais wa Sudan Omar al-Bashir anatarajiwa kuwasili mjini Juba kwa mazungumzo na Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir kuhusu mapigano yanayotokota nchini humo.
Vita vimekuwa vikiendelea nchini humo kwa zaidi ya wiki tatu huku pande zinazozozana zikikutana nchini Ethiopia kujaribu kukubaliana juu ya kusitisha vita.
Hadi sasa pande hizo hazijakubaliana chochote.
Mgogoro huo ni kati ya jeshi la serikali ya Rais Kiir na waasi wanaomuunga mkono aliyekuwa makamu wake Riek Machar.
Takriban watu 1,000 wameuawa tangu mapigano kuanza tarehe 15 Disemba
Vita vilianza baada ya Rais wa Sudan Kusini kumtuhumu bwana Machar kwa jaribio la mapinduzi, madai aliyoyakanusha.
Takriban watu 200,000 wameachwa bila makao,kutokana na vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe vinavyosemekana kutokana na ukabila.
Aidha Bwana Kiir anatoka kabila la Dinka naye hasimu wake bwana Machar akitoka katika kabila la Nuer.
Vyombo vya habari Sudan Kusini viliripoti kuwa Rais Bashir atakwenda Juba Jumatatu kujadiliana na Rais Kiir kuhusu mzozo huo ingawa hakuna taarifa zaidi zilizotolewa.
Awali msemaji wa wizara ya mambo ya nje mjini Khartoum alisisitiza kuwa Sudan ingependa kuona kipindi salama cha kutafuta mwafaka wa amani Sudan Kusini.
Hadi Ijumaa wiki mwishoni mwa wiki, mazungumzo ya amani mjini Addis Ababa,Ethiopia, yamekuwa yakiendeshwa na wapatanishi. Lakini sasa pande zinazozozana zinatarajiwa kuanza mazungumzo ya ana kwa ana.

Source:bbc

Ijumaa, 3 Januari 2014

Kwetu Mbambabay ndivyo kulivyo, angalia hapa

 Blogger wetu (kushoto) akiwa na mdau, Philipo pembezoni mwa ufukwe (Beach) ya  Mbamba bay
 Blogger Daniel Mkate akiwa mchangani katika ufukwe wa Mbamba bay
 Mvuvi akiwa na mtumbwi akitoka kusaka kitoweo cha samaki katika ufukwe wa Mbambabay
Wadau wakiwa katika mitaa ya Mbamba bay wakielekezana jambo