WAREMBO
16 kutoka Vyuo Vikuu mbalimbali nchini, wanatarajiwa kushiriki shindano la kumsaka
Miss Redd’s Highland, linalotarajiwa kufanyika Julai 5 mwaka huu ukumbi wa SAN SIRO Shekilango Jijini Dar es
Salaam.
Mratibu wa shindano hayo, Agnes Mathew alisema washiriki
hao wamepatikana baada ya kupata nafasi kutoka vyuo wanavyosoma.
“Tumejipanga
vizuri katika shindano hili, kwani washiriki wote wanaendelea kunolewa na
mwalimu Bless Ngowi, na kujiweka swa siku hiyo ya Ijumaa pale San-siro
Shekilango,” alisema Mathew.
Mratibu
huyo alisema mpaka sasa zawadi za washindi bado hazijatangazwa kutokana na
kuwasubiri wadhamini waliojitokeza kudhamini shindano hilo la kila mwaka.
Alisema ingawa mwaka jana mshindi wa kwanza alipewa Sh.mil. 2, Sh.mil.1.5 kwa wa pili na wa tatu mil.1, lakini mpaka sasa wadhamini hajawasema lolote kuhusu zawazi za washindi.
Mathew
aliwataja baadhi ya washiriki wa shindano hilo la ulimbwende ni Sia Mtui, Feube
Urio, Rosemary Alloyce, Nyangeta Kuboja, Avelyne Mathew, Juliet Msacky na
Severin Minga.
Katika
shindano hilo wasanii wa Bongofleva, Ney wa Mitego na Richie Mavoko watawasindikiza
warembo hao.
Aidha,
alisema wadhamini waliojitokeza katika shindano hilo ni pamoja na Redd’s,
EATV/Radio, Ngorongoro Conservation, Lake Gas, Coca-Cola, Clouds, Times FM,
Grand Villa Hotel, Shamool hotel, Sibuka na Magic fm.