Mwanachama wa chama cha
wafanyakazi ameuawa katika mgodi wa madini ya Platinum unaomilikiwa na
kampuni ya Lonmin ya nchini humo, huku kukiwa na hali ya taharuki
kati ya vyama hasimu vya wafanyakazi.
Chama cha kitaifa cha wafanyakazi wa migodini,
(NUM), kimesema kuwa mauaji hayo yalifanyika karibu na mji wa Marikana,
umbali wa kilomita 120 Kaskazini Magharibi mwa Johannesburg.Wakati huohuo, kampuni moja ya Uswizi imeelezea kuwa iliwafuta kazi wafanyakazi elfu moja waliofanya maandamano katika moja ya kiwanda chake wiki jana.
Migodi nchini Afrika Kusini, imekumbwa na mizozo tangu mwaka jana na kutishia imani ya waekezaji katika nchi hiyo.
"mmoja wa wanachama wetu, alishambuliwa kwa bunduki katika ofisi yetu ya Lonmin Magharibi mwa nchi,'' alisema msemaji Lesiba Seshoka.
Bwana Seshoka alisema kuwa hajui nani aliyefanya mauaji hayo.
Takriban watu 50 waliuawa mwaka jana katika migomo iliyokumbwa na ghasia kati ya vyama hasimu vya wafanyakazi na kile cha wajenzi.
Kundi moja linatuhumu lengine kwa kuwa na uhusiano wa karibu sana na wasimamizi wakuu wa serikali , tuhuma iliyokanushwa vikali.
source: bbc