http://www.mkcomputertweaks.com/mkgroup/fkbmksb.gifMatangazo

Tangaza nasi: mkatedaniel@gmail.com, +255 7666-00 69 70, +255 655-00 69 71, +255 787- 249594

Usilikose kila Jumapili

Ijumaa, 21 Juni 2013

DAVID Beckham azusha vurugu China



KUMETOKEA hamaniko kubwa katika chuo kikuu cha China wakati Balozi anayepeleka ujumbe wa ustaraabu katika soka na kuondokana na rushwa David Beckham alipojitokeza.Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya taifa ya England ambaye yuko China kwa ziara ya siku nne akinadi ustaarabu katika soka, alisababisha msukosuko mkubwa wakati alipojitokeza katika viwanja vya chuo kikuu cha Shanghai Tongji ili kukutana na timu ya chuo hicho.

Wakati akiingia katika eneo la chuo hicho, watu zaidi ya 1000 waliojipanga kumuona waliwazidi nguvu polisi, kuvunja ukuta  hali iliyosababisha hekaheka kubwa aliyoleta majeruhi.