http://www.mkcomputertweaks.com/mkgroup/fkbmksb.gifMatangazo

Tangaza nasi: mkatedaniel@gmail.com, +255 7666-00 69 70, +255 655-00 69 71, +255 787- 249594

Usilikose kila Jumapili

Jumamosi, 15 Juni 2013

MCHECHETO WA KUCHEZA NA STARS, TEMBO WAPIGANA WENYEWE


Mchezaji Jean-Jacgues Gosso Gosso (mwenye rasta) akimpiga kabali 'yosso' Abdul Razak huku Yaya Toure (kifua wazi) akijaribu kupangua kabali.


Wakati kesho timu ya taifa ya Tanzania, TAIFA STARS, ikiwa katika kibarua kigumu cha kucheza na timu ya taifa ya Ivory Coast, TEMBO, ndani ya uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam, wachezaji wawili wa timu hiyo ya Kaskazini mwa Afrika, walipigana kabali wakiwa mazoezini muda mchache kabla hawajapanda ndege  kuja DAR.

Mastaa waliokunjana ikionekana ni ishara ya mchecheto dhidi ya STARS ni mchezaji Jean-Jacgues Gosso Gosso anayechezea Mersin Idmanyurdu ya Uturuki na dogo wa Manchester City ya England, Abdul Razak, ambaye hata hivyo alitimuliwa katika kikosi kilichosafiri kwenda Tanzania, akionekana ndiye chokochoko.

Hata hivyo, ugomvi huo uliotaliwa na kabali 'sana', uliamuliwa na kiungo wa Man City, Yaya Toure, aliyefanya kazi ya ziada kunyofoa kabali ya Gosso Gosso dhidi ya Razak.

Timu hiyo inakabiliana na Stars katika mechi itakayopigwa Jumapili kuanzia saa 9 alasiri, kuwania moja ya nafasi 10 za mtoano ili kupata nafasi tano za kwenda BRAZILI kucheza fainali za Kombe la DUNIA 2014.