JUMLA ya warembo 23
wamejitokeza kushiriki katika shindano la kumtafuta Miss Tabata 2013 ambalo litazinduliwa
siku ya Pasaka kwenye ukumbi wa Da’ West Park Tabata.
Mratibu wa shindano hilo,
Joseph Kapinga alisema jana warembo hao watatambulishwa pamoja na wale
wanaoshiriki Miss Mzizima siku ya sikukuu ya Pasaka Da West Park.
Kapinga aliwataja warembo waliojitokeza
kuwania taji la Miss Tabata 2013 na kuendelea na mazoezi Da West Park ni Martha
Gewe (19), Zilpha Christopher (19), Hidaya David (22), Aneth Ndumbalo (19),
Amina Ally (18), Dorice Mollel (22), Eunice Nkoha (19), Kazunde Kitereja
(19), Angela Fradius (19), Domina Soka
(21), Rehema Kihinja (20), Glory Jigge (18) na Sophia Claud (21).
Aliwataja wengine ni Lilian
Mpakani (19), Lilian Msanchu (19), Rita Frank (20), Pasilida Mandali (21),
Rachel Mussa (19), Jasmin Damian (18), Angelina Mkinga (19), Mercy Mwakasungu
(20), Tunu Hamis (19), Blath Chambia (23), Ray Issa (22), Shamim Abass (22) na
Shan Abass (22).
Utambulisho wa warembo hao,
utasindikizwa na burudani kabambe kutoka bendi ya Twanga Pepeta “Wazee wa
Kisigino”.
Kapinga alisema wapenzi wa tasnia
ya urembo Jijini Dar es Salaam, watapata fursa ya kuwaona warembo kabla ya Miss
Tabata kufanyika Mei mwaka huu.
Miss Tabata 2013
imedhaminiwa na Konyagi, CXC Africa, Fredito Entertainment na Saluti5 na
kuandaliwa na Bob Entertainment na Keen Arts.
Washindi watano kutoka
Tabata watafuzu kushiriki Miss Ilala baadaye mwaka huu.
Anayeshikilia taji la Miss
Tabata ni Noela Michael ambaye pia ni Miss Ilala.