http://www.mkcomputertweaks.com/mkgroup/fkbmksb.gifMatangazo

Tangaza nasi: mkatedaniel@gmail.com, +255 7666-00 69 70, +255 655-00 69 71, +255 787- 249594

Usilikose kila Jumapili

Jumatano, 29 Mei 2013

JIDE, MwanaFA + KALAPINA WAPISHA MSIBA WA NGWEAR



 Lady Jaydee

2. 
                                                             MwanaFA



3.

                                                              Kalapina.
MWANADADA mkali wa miondoko ya muziki wa kizazi kipya nchini, Lady Jaydee a.k.a Anaconda, ameamua kufuta onyesho lake la miaka 13 tangu awe katika fani hiyo lililokuwa lifanyike Ijumaa hii, ili kuweza kupisha msiba wa Albert Mwangwea 'Ngwair' aliyefariki jana Sauzi Afrika.
Hatua ya Jide imeenda sambamba na ile ya wakali wengine wa muziki huo nchini MwanaFA ‘Binamu’ na Kalama Masoud 'Kalapina' ambao nao walikuwa wafanye maonyesho yao nao Ijumaa wiki hii katika Jijini Dar katika kumbi tofauti.
Jide amesema onyesho hilo halitafanyika wiki hii mpaka msiba wa Ngwair utakapomalizika.
Akihojiwa katika kipindi cha Super Mix kinachorushwa na kituo cha EA Radio, Jide ama ukipenda unaweza kumuita Komandoo au Binti Machozi, alikuwa na wakati mgumu alipoulizwa jinsi anavyomfahamu Ngwear.
Jide aliyekuwa mwenye huzuni akijibu huku akitokwa machozi akama lilivyo jina lake ‘Binti Machozi, amesema Tanzania imempoteza msanii nyota. Kuhusu shoo yake, Jide amesema imembidi aisogeze mbele mpaka msiba huu uishe ndipo atataja tena tarehe rasmi ya shoo yake.
Ngwair amefariki jana huko Afrika Kusini kwa kile kinachodaiwa kula chakula chenye sumu sambamba kujidunga sindano ya dawa za kulevya akiwa na rafiki yake M to the P aliyefariki leo na miili yao kuhifadhiwa hospitali ya Mtakatifu Hellen Jijini Johannesburg.