Lady Jaydee
2.
MwanaFA
3.
Kalapina.
MWANADADA mkali wa miondoko ya
muziki wa kizazi kipya nchini, Lady Jaydee a.k.a Anaconda, ameamua kufuta
onyesho lake la miaka 13 tangu awe katika fani hiyo lililokuwa lifanyike Ijumaa
hii, ili kuweza kupisha msiba wa Albert Mwangwea 'Ngwair' aliyefariki jana
Sauzi Afrika.
Hatua ya Jide imeenda sambamba na
ile ya wakali wengine wa muziki huo nchini MwanaFA ‘Binamu’ na Kalama Masoud
'Kalapina' ambao nao walikuwa wafanye maonyesho yao nao Ijumaa wiki hii katika
Jijini Dar katika kumbi tofauti.
Jide amesema onyesho hilo
halitafanyika wiki hii mpaka msiba wa Ngwair utakapomalizika.
Akihojiwa katika kipindi cha Super
Mix kinachorushwa na kituo cha EA Radio, Jide ama ukipenda unaweza kumuita Komandoo
au Binti Machozi, alikuwa na wakati mgumu alipoulizwa jinsi anavyomfahamu Ngwear.
Jide aliyekuwa mwenye huzuni akijibu
huku akitokwa machozi akama lilivyo jina lake ‘Binti Machozi, amesema Tanzania
imempoteza msanii nyota. Kuhusu shoo yake, Jide amesema imembidi aisogeze mbele
mpaka msiba huu uishe ndipo atataja tena tarehe rasmi ya shoo yake.
Ngwair amefariki jana huko Afrika
Kusini kwa kile kinachodaiwa kula chakula chenye sumu sambamba kujidunga sindano
ya dawa za kulevya akiwa na rafiki yake M to the P aliyefariki leo na miili yao
kuhifadhiwa hospitali ya Mtakatifu Hellen Jijini Johannesburg.