MSANII
wa muziki wa Bongofleva nchini, Amin anatarajiwa kutambulisha rasmi kibao chake
kipya kiitwacho ‘Nipoze roho’ baada ya kumalizika kwa tuzo za Kili Juni 11.
Akizungumza
na Kwety Mbamba-Bay, Amin anayetamba na kibao ‘Mtima Wangu’ alichomshirikisha
Linah, alisema kibao hicho kimeandaliwa katika studio ya Sir round ya jijini
Dar es Salaam chini ya prodyuza Ima ze Boy.
“Kwa
sasa naangalia kwanza tuzo za Kili, kisha baada ya kumalizika kwake Juni 8,
siku tatu za mbele nitatambulisha kibao hiki kipya ili kiweze kuruka hewani,”
alisema Amin.
Hata
hivyo, Amin alisema kwa sasa yupo katika mchakato wa kuhamasiaha mashabiki wake
wampigie kura katika tuzo hizo kupitia kibao alichoimba na Linah kikiwa katika
mahadhi ya zouk.