Na Boniface Wambura, Kampala
KIUNGO
mshambuliaji wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Khamis
Mcha ‘Vialli’ anaweza kuikosa mechi dhidi ya Uganda keshokutwa kuwania
tiekti ya kucheza Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN),
zinazohusisha wachezaji wanaocheza ligi za nchini mwao pekee dhidi ya
Uganda, The Cranes.
Kiungo
huyo wa Azam FC anaweza kuikosa mechi hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja
wa Mandela, Namboole kutokana na kusumbuliwa na maumivu ya goti.
Wachezaji
wengine wote wa Stars wako katika hali nzuri na hata Mcha aliyekuwa,
Dadktari wa timu, Mwanandi Mwankemwa amesema anaendelea tayari na
wanampa mazoezi mepesi.
Kikosi
cha kamili cha Stars ilichoko hapa kinaundwa na makipa Juma Kaseja,
Mwadini Ali na Ali Mustafa. Mabeki ni Aggrey Morris, David Luhende,
Erasto Nyoni, Kelvin Yondani, Nadir Haroub na Vincent Barnabas.
Viungo
ni Amri Kiemba, Athuman Idd, Frank Domayo, Haruni Chanongo, Khamis
Mcha, Mudhathir Yahya, Salum Abubakar na Simon Msuva. Washambuliaji ni
John Boko, Juma Luizio na Mrisho Ngasa.
Stars
iliwasili Kampala jana jioni tayari kwa mechi ya kuwania tiketi ya
CHAN, Fainali ambazo zitafanyika mwakani nchini Afrika Kusini.
Stars
ambayo iliwasili ikitokea jijini Mwanza ilipokuwa imepiga kambi ya siku
kumi kujiandaa kwa mechi hiyo itakayoamua ni timu ipi kati ya hizo
mbili itakwenda Afrika Kusini mwakani imefikia hoteli ya Mt. Zion
iliyoko eneo la Kisseka katikati ya Jiji la Kampala.
Kocha
Mkuu wa Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager, Kim
Poulsen ameridhishwa na kiwango cha hoteli hiyo, kwani ndiyo ambayo timu
ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) ilifikia Novemba mwaka jana
ilipokuja Kampala kushiriki michuano ya Kombe la Chalenji inayoandaliwa
na Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).
Stars
ambayo ilitiwa chachu na Rais Jakaya Kikwete alipokutana nayo Uwanja wa
Ndege wa Mwanza wakati ikiondoka kuja Kampala, na kuitakia kila la
kheri itafanya mazoezi yake ya mwisho kesho (Julai 26 mwaka huu) Uwanja
wa Mandela kujiandaa kwa mechi ya Jumamosi.
Kocha
Kim amesema ingawa mechi hiyo ni ngumu, lakini kikosi chake kimejiandaa
kuikabili Uganda kwani wachezaji wako wako vizuri na ari kwa ajili ya
mechi iko juu.
Wakati
huo huo, Kocha Kim Poulsen atakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari
siku ya Jumatatu (Julai 29 mwaka huu). Mkutano huo utafanyika saa 5
kamili asubuhi katika ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania (TFF).
IMEWEKWA JULAI 25, 2013 SAA 8:10 MCHANA