Golikipa mstaafu aliyedakia timu ya taifa Tanzania katika mashindano ya African Cup Of Nations 1980, Juma Pondamali 'Mensah', ambaye kwa sasa ni kocha wa makipa wa timu ya taifa 'Taifa Stars', ameingia rasmi kwenye orodha ya
wasanii wa Bongofleva ambao wamewahi kuchezea ligi kuu ya Tanzania.
Unashangaa!!!!! ndio namaanisha Juma Pondamali, ameachia wimbo wake unaoitwa "Pesa Inatutesa"
Pondamali enzi zake akiwa uwanjani alisifika kwa udakaji wa mbwembwe uwanjani na amewahi kufungiwa kucheza soka mara 5 huku mara 4 mechi alizocheza dhidi ya timu yake, zilivunjika kwa sababu yake.
Msanii huyo amezungumzia pia kama kutakuwa na muendelezo baada ya kuachia ngoma hii, lini alijua kama ana uwezo wa kufanya mziki maana
mmmmmhhhhhh!!!!!
Licha ya timu ya taifa, Pondamali amezichezea Pan Afrika na Yanga Sports Cluba zote za Jijini Dar es Salaam.
huu ndio wimbo wake unaoitwa "Pesa inatutesa"