WASANII wa muziki wa BONGOFLEVA nchini, Juma
Nature, Mkoloni na mapacha wa Ant-virus kwa pamoja wameibuka na kibao kipya
kiitwacho ‘Alisema Mwalimu’ kilichotokana na milipuko ya mabomu ya mara kwa
mara nchini.
Nature amesema kibao hicho kimerekodiwa Halisi Records na
kuwashirikisha wasanii hao walioungana kwa pamoja kuzungumzia wosia wa Hayati
Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kuhusu taifa la Tanzania.
“Tumeshirikiana kwa
pamoja katika kibao hicho ili kuelezea hisia zetu na meseji aliyoiacha Baba wa
Taifa kuhusiana na amani ya nchi yetu…hivyo kibao hiki cha ‘Alisema Mwalimu’
kitafikisha ujumbe,” alisema Nature ambaye kwa sasa ni prodyuza.
Aidha, alisema
katika kuelekea mfungo wa Ramadhani, kundi lake la Wanaume Halisi halitakuwa
likifanya shoo yoyote hadi hapo siku 30 za kufunga zitakapokamilika.