http://www.mkcomputertweaks.com/mkgroup/fkbmksb.gifMatangazo

Tangaza nasi: mkatedaniel@gmail.com, +255 7666-00 69 70, +255 655-00 69 71, +255 787- 249594

Usilikose kila Jumapili

Jumanne, 23 Julai 2013

MSANII BONGO MOVIE AVUNJIKA MIGUU AKIEKTI MOVIE KWA KUJIRUSHA GHOROFANI


Na Livingstone Mkoi
Msanii nyota toka kiwanda cha muvi za kibongo nchini Maulidi Mfaume maarufu kwa jina la Gado Balotel sasa amekumbwa na balaa la aina yake baada ya kuvunjika miguu yote miwili pamoja na nyonga kuteguka baada ya kudondoka toka ghorofa ya nne alipokuwa akiigiza filamu ya msanii mwingine aitwae Baga.

Baada Xdeejayz na kituo cha luninga cha DTV kupata taarifa hizo lilipiga hatua ndefu hadi mahala anapojiuguzia msanii huyo ambako ni nyumbani kwa msanii Wilson Fike maeneo ya Home Alone Vijana Kinondoni na kuonana uso kwa uso na msanii huyo aneyeishi na maumivu makali.

Akiongea na mwandishi wetu nyumbani hapo Balotel alisema alikutwa na balaa hiyo wiki mbili zilizopita akiwa Location ndani ya hotel ya Conway iliyopo Magomeni Kagera na wasanii wenzake kama Hemed, Baga, Manaiki Sanga na wengineo wakati wakiigiza.

Balotel aliendelea kusema wakati shughuli za kuigiza ziliendelea na kuna sini moja iliyokuwa inahitajika kuigizwa kwa mfano ikimtaka mtu aigize kama anataka kujirusha kwenye ghorofa lakini asiruke ili kameraman achukue picha achukue shoti hiyo kisha mtu huyo aende chini kisha achukuliwe shoti nyingine ya kujifanya ametua chini.
Msanii huyo aliendelea kusema kuwa nafasi hiyo ilibidi aigize msanii mwenye filamu Baga lakini kutokana na uwoga wa msanii huyo alikuwa akijishauri namna ya kuigiza kuruka ghorofani ndipo Balotel akamtoa pembeni na kumuonesha namna ya kuruka kama Jet Lee huku akimwambie mwenzake hiyo ilikuwa kazi ndogo sana.

Msanii huyo aliendelea kusema kuwa baada ya hapo alijikuta ameruka toka ghorofa ya nne, lakini aliendelea kusema“ Wakati nikiwa bado sijashuka chini njiani nilianza kuhisi harufu ya kifo kwani tayari nimuona Israel mtoa roho akinipungia mkono na hatimaye nilitua chini kwa kufikia miguu,” alisema Ballotel

Hata hivyo, kijana huyo aliongeza kusema kuwa mara baada ya kutua chini alihisi moto unawaka miguuni mwake huku harufu ya damu ikimtoka puani na mdomoni na baada ya kujiangalia aliona visigino vyake vikiwa vimepasuka vyote huku tumboni kukiwa na maumivu makali sana kumbe wakati huo nyonga ilikuwa imeachia huku miguu yake ikiwa imesogea tumboni.

Gado alisema baada ya tukio hilo wasanii wenzake walimchukua na kukmimbiza Hospital ya Mwananyamala mbapo dakika chache baadae walimkimbiza Muhimbili kwa matibabu zaidi. Msanii huyo ambaye ametamba sana kwenye filamu kama Going Bongo, Msitu wa Hifadhi,Tumbo Joto na Escap ambayo alikuwa akiigiza siku ya tukio lililomkuta.
Aidha, msanii huyo aliendelea kusema kwa sasa anaishi akiwa na mateso makali huku wasanii wenzake wakishindwa kumpa ushirikiana.

“Hapa nilipo nalelewa na Fike Wilsoni ambaye ananibeba kwenda chooni na kunirudisha kwa kweli hali yangu sio nzuri nahitaji msaada wa wasanii wenzengu, wako wanaokuja kunirushia chochote kama Kalapina,Young Killer na madaktari wanasema huenda wakanishauri kwenda India ili wakazirekebishe nyonga zangu” Alisema Gado na kuongeza kuwa anawaomba wasanii wenzake wasamaria wema kumsaidia kwani hali yake ni mbaya na huenda kwa mujibu wa madaktari wake akahitajika kupelekwa India ili kukinusuru kiuno chake la sivyo hatozaa tena kwa vile nyonga vimeshafyatuka.