http://www.mkcomputertweaks.com/mkgroup/fkbmksb.gifMatangazo

Tangaza nasi: mkatedaniel@gmail.com, +255 7666-00 69 70, +255 655-00 69 71, +255 787- 249594

Usilikose kila Jumapili

Ijumaa, 22 Novemba 2013

NGUGI WA THIONG'O AWAUMBUA VIONGOZI WA KIAFRIKA KUTOENZI LUGHA ZAO

Mwanazuoni na Mwanafasihi mahiri Duniani, Ngugi wa Thiong'o amewaumbua wasomi na viongozi wa Afrika kwa kukimbilia lugha za kigeni na kutoenzi zile za Kiafrika.
Ngugi ametoa Muhadhara leo katika CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (UDSM).

 1. Prof. Ngugi wa Thiong'o akitoa mhadhara katika ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam leo.
 2. Ngugi wa Thiong'o
 3. Ngugi akiendelea kutoa mhadhara kwa lugha ya Kiswahili
 4. Ngugi akifurahia jambo
 5.Baadhi ya washiriki katika mhadhara uliotolewa na mwanazuoni Ngungi wa Thiong'o
 6. Watu mbalimbali wakiwemo Maprofesa na wahadhili mbalimbali wakimfuatilia kwa makini Ngugi
 7. Hawa nao walikuwepo
  8. Juu na chini ya ukumbi wa Nkrumah walifurika watu kumsikiliza mwanazuoni na mwanafasihi Ngugi wa Thiong'o

Jumatatu, 18 Novemba 2013

IBADA KUTOKA NYUMBA YA UFUFUO NA UZIMA KAWE DSM NA MCHUNGAJI KIONGOZI JOSEPHAT GWAJIMA

IBADA KUTOKA NYUMBA YA UFUFUO NA UZIMA KAWE,DSM NA MCHUNGAJI KIONGOZI JOSEPHAT GWAJIMA

Mch.Kiongozi Josephat Gwajima
SOMO: VITA NA WALIOKUFA KATIKA DHAMBI
Jumapili Tarehe 17.11.2013

Na Mch. Josephat Gwajima

Nimeamua kuliita hili somo vita sababu tunakwenda kupigana vita moja kwa moja na majeshi ya wafu waliokufa katika dhambini

1 Samwel 28:6-20

“…Ukanipandishie yeye nitakaye mtaja kwako…” tunaoana hapa mfalme anakwenda kwa mganga wa kienyeji anaomba apandishiwe mtu aliekufa miaka mingi, Hapa tunaona kumbe mtu aliekufa anaweza kupandishwa na waganga wa kienyeji kutoka kuzimu na akapanda/akazuka.  
1 Samwel 28:11 “…Nipandishie Samwel...” hapa tunaona Samwel alikuwa amekufa lakini mfalme sauli anamwambia mganga wa kienyeji nipandishie Samweli. 
1 Samwel 28:15 “…Ndipo Samwel akapanda na akamwambia mbona umenitaabisha mimi hata kunipandisha juu...”  Kumbe mtu aliekufa anaweza akapandishwa na akazuka kikweli kweli (Samweli akazuka juu),  
1 Samwel 28:19 “….Tena pamoja na wewe Bwana atawatia Israel mikononi mwa Wafilisti; hata na kesho wewe na wanao mtakuwepo pamoja nami…” Haya ni maelezo anayoyatoa Samweli baada ya kuzuka juu. Akatoa maelezo kwamba baada ya siku tatu utakufa wewe na wanao na mtakuwa mahali hapa name, yaani na nyie mtapandishwa kama mlivonipandisha mimi.

Ukisoma theolojia kuna ubishani mwingi unaendelea, wanatheolojia wengi wanasema sababu Samwel alikuwa mtu wa Mungu, sasa ilikuaje mpaka mganga wa kienyeji akaweza kumpandisha, hivyo husema huyu hakuwa Samweli bali ni pepo (Samweli feki). Lakini mimi nataka nikuambie kuwa huyo alikuwa ni Samweli mwenyewe ndio maana aliweza kumpa maelezo mengi sana, ikiwemo kwamba wewe umemuacha Bwana, na umeamua kunitaabisha kunipandisha juu, hivyo baada ya siku tatu wewe na familia yako mtakufa.

Mfalme Sauli alipoona hajibiwi kwa maono wala kwa ndoto, ndio maana akaamua aende kwa mganga wa kienyeji, ndio maana mimi huwa na kwambia kila kiongozi ambaye hajaokoka anamganga wake wa kienyeji, Mwanadamu kwa asili huwezi ukawa mtupu, ni lazima uwe umeungamanika na madhabahu ya mwanakondoo ama madhabahu ya lusifa. Mimi mwenyewe unavyoniona hapa kuna mamlaka nyuma yangu nimeungamanishwa nayo. Usifikiri leo Ufufuo na Uzima tupo hivi, ukadhania tumeibuka buka tu, hapana kuna vita huko nyuma tumepigana.


Sauli amekwenda kwa mganga wa kienyeji akaomba apandishiwe Samweli ili amuulize limpasalo kutenda. Sauli alijificha ili asijulikana na mganga wa kienyeji kama ni mfalme, maana wafalme walikuwa hawaruhusiwi kwenda kwa waganga wa kienyeji. Baada ya mganga wa kienyeji kuanza kumpandisha Samweli alipiga kelele, akamwambia mbona umenidanganya, (mganga wa kienyeji viliumana na samweli alivokuwa anazuka), Sauli akauliza kwanai anayezuka ni nani akamwambia akasema ni mzee anamavazi meupe anazuka katika nchi. Hapo usifikiri kiliwekwa kikopo cha maji, Sauli akamuona Samweli kwenye maji hapana, Samweli alipanda akaanza kuongea ndani ya mganga wa kienyeji. Inanifurahisha hiimaana mganga wa kienyeji badala ya kupandisha vibwengo akapandisha Samweli, na Samweli akatoa maelekezo.

Mchungaji Kiongozi,Josephat Gwajima, akihubiri ndani ya nyumba ya ufufuo na uzima, Kawe, Dar es Salaam

Watu wakifa wanakwenda wapi?

Kabla Yesu hajafa msalabani kuna sehemu ilikuwa inaitwa shiol hili neno ndio hilo limetafsiriwa na biblia linaitwa kuzimu, yaani ulimwengu wa wafu, ama eneo wanalokaa wafu. Waliokufa katika dhambi ama waliokufa katika haki. Shiol ilikuwa imegawanyika sehemu mbili shiol ya watu waliokufa katika haki na shiol ya watu waliokufa katika dhambi, na hii ilikuwa kabla Yesu hajafa msalabani.  
Mwanzo 37:35 “…Nitamshukia mwanangu hata kuzimu nikiwa nasikitika…” Yaani hapa Yakobo anamaanisha akifa atamshukia mwanae Yusufu huko kuzimu, hii ilikuwa ni kuzimu ya waliokufa katika haki.  
Torati 32:22 “…Moto umewashwa kwa hasira yangu unateketea hata chini ya kuzimu…” Hii ni kuzimbu ya waliokufa katika dhambi.

“Kusimu upande wa wenye haki, na kuzimu upande wa waliokufa dhambini Kabla ya Yesu Kristohajafa msalabani”

1 Samweli 2:6 “…Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu…” Zaburi 6:5 “…Maana mautini hapana kumbukumbu lako; katika kuzimu ni nani atakayekushukuru?...” Zaburi 16:10 “…Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu…” Yuda 1:6 “...Amewaweka vifungo vya milele chini ya giza…” kuzimu kwa lugha ingine ni chini ya giza kwenye vifungo vya milele.

Yesu alipokufa akashuka kuzimu ya waliokufa katika dhambi akamnyang’anya yule joka ufunguo wa kuzimu na mauti, halafu akaeleke upande wakuzimu ya Ibrahimu (kuzimu ya walikufa katika haki) akawaambia yule uzao wa mwanamke ndio mimi, akawahubiria manabii wote huko kuzimu, na kuwaambia nimekuja kuwahamisha twende juu mbinguni, huku sio mahala penu. Yale makaburi kufunguka ilikuwa ni ishara ya uhamisho wa watu wote waliokufa katika haki kutoka kuzimu ya chini na kwenda mbinguni (paradiso) kule Yesu anakaa. Yesu akawaambia sasa tunahama huku tunaenda paradiso. Kwa hiyo baada ya hapo kuzimu ikawa ni mahali pa wafu waliokufa kwatika dhambi na paradiso (mbinguni) ikawa ni makao ya waliokufa katika haki huko wakimuimbia Mungu,na kufurahi.

Sasa kama vile Samweli alivyopandishwa kutoka kuzimu, kaganga kamama kakampandisha Samweli juu, hivyo ndivyo ambavyo leo mtu aliekufa katika dhambi inawezekana akaitwa na waganga wa kienyeji na akaja, wakamtumia kuharibu ukoo kama wawezavyo, Samweli alipanda lakini mganga alishindwa kumpa maelekezo sababu alikuwa mtakatifu akiwa duniani, lakini mababu na mabibi waliokufa katika dhambi wakipandishwa wanaamrishwa wafanye kile mganga anataka.


Kama tulivyoona aliekufa katika haki akaenda mbinguni, humuimbia Mungu na kufurahi huko mbinguni, na wale waliokufa katika dhambi hushuka kuzimu (kifungoni) na kutumika kwa kazi za kuzimu. Na ndio maana leo nasema lazima tupigane nao vita.

Unapokata roho huwa kuna malaika maalumu wanaochukua roho yako, kama ulikuwa unatenda dhambi malaika wa giza wanabeba roho yako wanashusha mpaka kuzimu(gereza la milele), na kama ulikuwa unatenda haki, malaika kutoka mbinguni wanabeba roho yako na kuipeleka mbinguni (pradiso), Ufunuo 20:13. “…Kuzimu ikawatoa watu waliokuwa ndani yake…” Kuzimu ni makao makuu ya shetani, na ziwa la moto ni sehemu ya hukumu ya wale waliokufa katika dhambi, ukishafika hapo unakuwa mfungwa, na unaanza kumtumikia shetani. Babu yako yule aliekufa katika dhambi yupo kuzimu hajakaa tu kule, yupo anapiga mzigo huko, ndio maana utasikia watu tunaowarudisha msukule hapa, ama watu waliokuwa wamekufa wakifufuka hapa kwetu utasikia kazi yangu ilikuwa ni kwenda kwenda kuua watoto wadogo mahosipitali wengine utasikia nilikuwa nasababisha ajali barabarani, hizo ndizo kazi za wafu huko kuzimu.

Mtu anajiuliza hivi watu wanawezaje kumtupia mtu mapepo hata 1000, unauliza huyu ana akiba ya mapepo kiasi gani, kumbe mengine sio mapepo bali ni watu waliokufa wanatumikishwa na shetani, wapo kuzimu lakini wanatumwa kuja duniani, na huwa wanatumwa kwenye koo zao kufanya uharibifu sababu wao wanazijua hizo koo zao vizuri, ni rahisi kushambulia kwa mafanikio makubwa. Kwanza wanafahamu lugha ya ukoo wenu, wanamfahamu baba wa ukoo, wanafahamu madhaifu yenu yote, ndio maana vita yako huwa inakuwa kali kweli. Shetani huwa anawatuma anawaambiakama vile wewe ulivyokuja huku katuletee shangazi yako, ndio maana utasikia watu wanalalamika bibi yangu alikufa kwa kansa na mama yangu nae kwa kansa na mimi nina kansa sasa hivi, huu ni ugonjwa wa ukoo! Hakuna ugonjwa wa ukoo ni wafu wanatenda kazi katika ukoo.

Makundi yanayoshambuliwa sana na majeshi ya wafu

1.   Wale wanaochukua majina ya ndugu wa ukoo ambao hawajaokoka (majina ya mabibi, mababu, shangazi).

Tuangalie sana majina tunayowapa watoto, utasikia mtu anamwita mtoto dragon, astrorogy, au momony angalia utalia, usimpe majina ya ndugu wa ukoo waliokufa watoto wako kama hujui maana yake, chagua majina yanayompa utukufu Mungu, Glory, Ruth, Grace….

Kwanini agano jipya linaanza na kutaja ukoo wa Yesu?

Hii walitaka kutuonesha kwamba ukoo wa Yesu hauna mganga wa kienyeji, wala msoma nyota, wala darweshi, wate walikuwa watu wa haki.

2.    Wale wanaopenda/wanaoendekeza  mila za familia

Utasikia desturi ya ukoo wetu ndugu yeyote anaekufa wote tutanyolewa vipara, mtoto akizaliwa lazima kitovu apewe shangazi, lazima tukajengee makaburi ya babu. Ukiwa unashiriki hizi taratibu lazima majeshi ya wafu yatakupata tu.

3.    Wale wanaopenda makabila kuliko kumpenda Mungu

Namna ya kuomba

Kwa jina la Yesu ninajitenga kabisa, na watu waliokufa kwenye dhambi. Mimi ni wa ukoo wa Yesu, ninajitenga na nyie kwa jina la Yesu. Jina lolote la mtu alielala katika dhambi, ninajitenga nalo kwa jina la Yesu

Jitenge na umasikini wa ukoo, umasikini wa bibi, umasikini wa babu, umasikini wa shangazi, jitenge na ukoo wako kwa damu ya Yesu, najitenga kutoka babu nababu na babu, nawaamuru muachie mali zangu, achia afya yangu, kata kamba zote za ukoo, kamba za familia kwa jina la Yesu.

NGOMA MPYA: DARASSA FT. MCHIZI MOX & SHILOLE - MIKONO JUU

NGOMA MPYA: DARASSA FT. MCHIZI MOX & SHILOLE - MIKONO JUU

Hii ni moja kati ya ngoma ambazo zipo ndani ya MixTape mpya inayoitwa Dream Big ya rapper Darassa ambayo ameachia Weekend hii.
Ambapo ngoma hii ya Mikono Juu ambayo amemshirikisha msanii Mchizi Mox pamoja na mwanadada Shilole ndio ngoma ya kwanza kabisa kati ya ngoma 19 ambazo zilizopo ndani MixTape hiyo.

Jumanne, 12 Novemba 2013

Kizungumkuti cha amani kati ya M23 na DRC

 12 Novemba, 2013 - Saa 05:15 GMT

DRC ilisusuia shughuli ya kutia saini mkataba wa amani kutokana na maandiko yake
Shughuli ya kutia saini mkataba wa amani kati ya waasi wa M23 na serikali na Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo,iliyokukuwa imepangwa kufanyika Jumatatu , iligonga mwamba.
Hii ni kutokana na serikali ya Congo kusema kuwa mkataba huo uangaliwe upya na hivyo kulazimisha shughuli hiyo kuahirishwa.
Mpatanishi wa pande hizo mbili Ofuono Opondo wa Uganda, alisema kuwa pande hizo hazikuwa tayari kuonana ana kwa ana baada ya DRC kusema kuwa M23 watie saini mkataba katika chumba tofauti na kisha wapewe wao kuusaini.
Hata hivyo mpatanishi alisema haiwezekeni kwa hilo kufanyika kwa sababu pande zinazozozana lazima zikae katika chumba kimoja kwa ajili ya kufanikisha juhudi za upatanishi.
Kundi la waasi la M23 lilisitisha uasi wao baada ya kupata kipigo kutoka kwa wanajeshi wa DRC wakisaidiwa na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa waliowafurusha kutoka maficho yao ya milimani katika mpaka wa Rwanda na Uganda.
Mkataba huo ulistahili kutiwa saini mjini Kampala Uganda, ingawa shughuli yenyewe ilicheleweshwa bila ya kujua itafanyika lini.
Mwandishi wa BBC mjini Kampala, Ali Mutasa anasema kuwa mpatanishi mkuu Ofwono Opondo alisema mkataba hautatiwa saini na kwamba haijulikani ni lini makubaliano hayo yatasainiwa. Alisema Upande wa M23 uko tayari kwa shughuli hiyo na kuwa kizungumkuti kimetokana upande wa DRC.
Serikali ya DRC kupitia kwa msemaji wake,Lambert Mende ilisema kuwa Kinshasa iko tayari kutia saini makubaliano hayo, lakini sio mkataba unaosema ni makubaliano ya amani kwa sababu ni kama kundi hilo bado lipo.
Duru zinasema kuwa Rais Yoweri Museveni pamoja na wanadiplomasia wa nchi za Magharibi, walisburi mkataba kutiwa saini lakini wajumbe wa DRC hawakuingia katika chumba cha hafla hiyo ya kutia saini.

Ijumaa, 8 Novemba 2013

MCHUNGAJI JOSEPHAT GWAJIMA WA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA AKABIDHIWA TUZO NA MAASKOFU


Umoja wa wachungaji wa makanisa ya Kipentekoste mkoani Kilimanjaro (PPK)wamempa tuzo ya heshima kanisa la Ufufuo na Uzima kwa mafanikio yao katika kumtangaza Kristo. Tuzo hiyo imekabidhiwa tarehe 30 mwezi uliopita ikiwa ni siku tatu toka kumalizika kwa mkutano mkubwa wa injili ulioandaliwa na mchungaji Gwajima chini ya kanisa lake katika viwanja vya mashujaa mjini Moshi.

Tuzo hiyo ya heshima yenye picha ya mlima Kilimanjaro ilitolewa na mchungaji kiongozi wa umoja huo Samweli Yohana katika ukumbi wa hosteli za Umoja kanisa la Kilutheri Moshi mjini. Mkutano wa wiki moja uliofanyika viwanja vya mashujaa mjini moshi ulivunja rekudi ya idadi ya wahudhuriaji na watu kutoka dini tofauti.

Picha zifuatazo ni matukio ya kukabidhiwa Tuzo hiyo





Alhamisi, 7 Novemba 2013

AKIMBIA MBWA MWITU ALIWA NA MAMBA

NGIRI AKIAMINI AMEWASEVU MBWA MWITU WALIOMZUNGUKA, LAKINI NYUMA YAKE MAMBA AKIFURAHIA KITOWEO (ANGALIA MSHALE). NGIRI HUYO HAKUWEZA KUSALIMIKA KWANI ALIISHIA MDOMONI MWA MAMBA

FOLENI KUBWA YA WAKAZI WA GONGO LAMBOTO WAKIJIANDIKISHA VITAMBULISHO VYA TAIFA

WAKAZI WA GONGO LA MBOTO WAKIWA KATIKA FOLENI YA NDEFU MAENEO YA KITUO KIPYA WAKISUBIRI KUJIANDIKISHA VITMABULISHO VYA TAIFA

Azam FC ya Tanzania yamtimua kocha Stewart

Stewart Hall kocha wa Azam FC

Huku ligi kuu soka Tanzania Bara ikiwa imekamilisha mzunguko wake wa kwanza hii leo,timu ya Azam FC ya Dar es Salaam imetangaza kusitisha mkataba na kocha wake mkuu Stewart Hall wa Uingereza kwa kile kilichoelezwa kama makubaliano ya pamoja.
Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa klabu hiyo jijini Dar es Salaam, hii itakuwa ni mara ya pili kwa kocha huyo kuachana na klabu ya Azam na ameafikiana na uongozi wa klabu hiyo baada ya kukamilisha mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo ambapo timu ya Azam sasa inashika nafasi ya Pili baada ya kwenda sare ya mabao 3-3 na timu ya Mbeya City ambapo zote sasa zina Pointi 27. Bingwa mtetezi timu ya Yanga inaongoza ligi hiyo kwa sasa ikiwa na pointi 28 baada ya kuinyuka Oljoro JKT mabao 3-0 katika mchezo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo, maaruf kama Vodacom Premier League.
Klabu ya Azam FC inayoinukia kwa ubora wa miundo mbinu huku ikiendeshwa kisasa kwa mipango inayoeleweka kinyume na klabu nyingi nchini Tanzania imekuwa ikifanya vema chini ya mwalimu huyo ambapo msimu uliopita aliiwezesha kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kushika nafasi ya Pili katika Ligi kuu msimu uliopita.
Klabu hiyo inao wachezaji kadhaa wa Kulipwa kutoka nchi za Ivory Coast, Kenya na Uganda. Kuachia ngazi kwa kocha huyo kunaelezwa kuwa kumekuwa kwa mkakati ili kusiathiri mwenendo wa timu hususan wakati ligi ikiendelea na sasa kutaiwezesha Azam FC Kutafuta kocha mwingine hususan wakati huu ambapo ligi imefikia mapumziko.
KATIBU MKUU MSAIDIZI WA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO, PROF. ELISANTE OLE GABRIEL, LEO ALITEMBELEA CHUO CHA FUTURE WORLD VOCATIONAL KILICHOPO ULONGONI 'A' GONGO LAMBOTO.
CHUO HICHO KINAFADHILIWA NA SHIRIKA LA PLAN INTERNATIONAL PAMOJA NA SERIKALI YA CANADA.

 Pro. Elisante ole Gabriel akizungumza jambo huku akimuonyesha mratibu wa fedha wa Plan International, Stella Tungaraza (kulia), wakati akizungumza na wanachuo wa Future World leo asubuhi.
 Wanachuo wa Future World wakimsikiliza kwa makini Prof. Gabriel.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Plan International ni miongoni mwa waliohudhuria hafla hiyo.
 Prof.Gabriel akisisitiza jambo.
 Prof. Gabriel akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi na wanachuo wa Future World leo chuoni hapo.
Simon Ndembeka (shati nyekundu) mmoja wa maafisa wa Plan International akiwa pamoja na katibu msaidizi, Prof.Gabriel wakionyesha ishara ya mshikamano na baadhi ya wanachuo wa Future World kilichopo Ulongoni A Gondo lamboto. (Picha zote: Daniel Mkate)

Jumanne, 5 Novemba 2013

MENDE: TUMEWAPIGA M23 KAZI IMEMALIZIKA


Lambert Mende Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imesema majeshi yake kwa kushirikiana na kile kikosi maalum cha Umoja wa Mataifa kilichopewa uwezo wa kupambana na waasi wa M23 kimewapiga waasi hao katika ngome yao ya mwisho.
Msemaji wa Serikali, Lambert Mende ameiambia BBC kuwa wapiganaji waliobaki wa M23 wanaweza wakawa wamekimbia, wamevuka mpaka au wamejisalimisha.
Mende amesema kikosi maalum cha majeshi ya nchi hiyo kimeharibu silaha za waasi hao usiku kucha na inasadikiwa kiongozi wa kijeshi wa kundi hilo la M23, Sultani Makenga ni miongoni mwa waliovuka mpaka na kuingia Rwanda au Uganda.
Wakati huo huo, viongozi wa nchi za SADC wanaokutana nchini Afrika Kusini wamezungumzia mgogoro wa Jumhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kuwataka viongozi wa kundi la waasi wa M23 kutangaza kusimamisha mapigano.
Taarifa iliyotolewa baada ya mkutano huo imesema kama waasi hao watachukua hatua hiyo mkataba wa amani unaweza kusainiwa ndani ya siku tano zijazo.

CHANZO: BBC