http://www.mkcomputertweaks.com/mkgroup/fkbmksb.gifMatangazo

Tangaza nasi: mkatedaniel@gmail.com, +255 7666-00 69 70, +255 655-00 69 71, +255 787- 249594

Usilikose kila Jumapili

Ijumaa, 6 Septemba 2013

ALIYEZIMIA MIAKA 19 AZINDUKA, HAELEWI KINACHOENDELEA


MTU mmoja aliyepata ajali na kuzimia kwa miaka 19 ameamka katika uzingizi wake na kujikuta akishangaa nini kinaendelea duniani.
Mtu huyo raia wa Poland alizimika wakati chama cha kikomunisti kipo madarakani na siasa ya ujamaa ikitawala na kuamka chama hicho kikiwa hakipo madarakani na ujamaa ukiwa umekufa.
Wakati anazimika chakula na umeme vilikuwa vikipatikana kwa resheni na kuamka kila mtu akiw abize kusaka chakula manake serikali haitoi tena wala haigawi kwa mfumo wa kila mtu awe nacho japo kidogo.
Televisheni ya Poland ilimuonesha mfanyakazi huyo wa zamani wa reli Jan Grzebski, 65, akielezea kushangaa kwake na mabadiliko aliyoyakuta baada ya kuamka.
Inadaiwa kwamba aligongwa na treni mwaka 1988.
Anaamini kuamka kwake kunatokana na mapenzi makubwa aliyokuwa nayo mkewe Getruda ambaye alikuwa anamhudumia kipindi chote cha yeye kuwa usingizini. Madaktari walisema kwamba nafasi ya kuishi kwa mtu huyo ni miaka miwili au mitatu tu.
Alisema kuamka kwake kumemfanya aone mabadiliko mengi na hasa kujaa kwa vituj madukani, watu wanatamba na simu za mikononi njiani hali inayomfanya aone kizunguzungu .
"Now I see people on the streets with mobile phones and there are so many goods in the shops it makes my head spin," he told Polish television.
A comatose patient is in a profound state of unconsciousness which renders them unaware of both self and the world around them, and from which they cannot be roused.
Although those in a coma do not respond to stimuli in a meaningful way, contrary to popular belief they do not always lie quiet and still - in some cases they can move, open their eyes and even talk.
Fall of communists
"It was Gertruda that saved me, and I'll never forget it," Mr Grzebski told news channel TVN24 of his recovery.
Mrs Grzebski is reported to have moved her husband every hour to prevent bed sores.
"I cried a lot, and I prayed a lot," Mrs Grzebski said on Polsat television.
"Those who came to see us kept asking: 'When is he going to die?' But he's not dead."
When Mr Grzebski had his accident Poland was still ruled by its last communist leader, Wojciech Jaruzelski.
"When I went into a coma there was only tea and vinegar in the shops, meat was rationed and huge petrol queues were everywhere," Mr Grzebski said.
The following year's elections ushered in eastern Europe's first post-communist government.
Poland joined the Nato alliance in 1999 and the European Union in 2004.
"What amazes me today is all these people who walk around with their mobile phones and never stop moaning," said Mr Grzebski.
"I've got nothing to complain about."

Jumatatu, 26 Agosti 2013

Goma Mashariki mwa Congo 'Kimenuka' tena


Raia wakibeba mwili wa mtu aliyeuawa Goma
 
Mapigano mapya yamezuka mwishoni mwa juma katika eneo la Goma, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo ripoti zinasema watu watatu walifariki baada ya makombora kurushwa katika maeneo ya makaazi ya watu.
Haijulikani ni nani aliyerusha makombora hayo lakini wanainchi wameandamana wakililaumu jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa MONUSCO kwa kile wanachodai limewashambulia waasi katika juhudi za kuwatimua kwenye eneo hilo.
Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wamewalaumu waasi kwa kurusha makombora hayo lakini hakuna kundi lolote la waasi ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo.
Afrika Kusini, ambayo imechangia kikosi hicho cha kulinda amani, imekiri kuwa mwanajeshi wake mmoja amejeruhiwa katika mlipuko huo wa bomu.
Akizungumza kwa simu na BBC, Msemaji wa jeshi la Afrika Kusini, Brigedia Generali Kolani Mabanga, amesema mwanajeshi wake mmoja alijeruhiwa vibaya na kwa sasa anaendelea kupata matibabu huku mipango ya kumrejesha nyumbani kwa matibabu zaidi ikiendelea.
Hali ya ulinzi imeimarisha katika eneo hilo lakini wakaazi wa mji huo na viunga vyake wanasema hali bado ni ya wasi wasi.

source; bbc

Jumamosi, 24 Agosti 2013

DHAIRA, OWINO, KAZE, TAMBWE WAKWAMA SIMBA KUCHEZEA VPL


Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imezuia usajili wa wachezaji 37 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kutokana na usajili wao kuwa na kasoro.
 Klabu husika zimetakiwa kurekebisha kasoro hizo kabla ya kuanza kuwatumia wachezaji hao kwenye mechi za VPL ambazo zinaanza leo (Agosti 24 mwaka huu) katika viwanja mbalimbali nchini.
 JKT Ruvu Stars inatakiwa kuwafanyia uhamisho (transfer) wachezaji Salum Machaku Salum aliyekuwa Polisi Morogoro na Emmanuel Leonard Swita (Toto Africans). Mgambo Shooting inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Mohamed Hussein Neto (Toto Africans), Kulwa Said Manzi (Polisi Morogoro) na Mohamed Ally Samata (African Lyon).
 Pia Salum Aziz Gilla anaonekana bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Coastal Union huku kukiwa hakuna vielelezo vyovyote kutoka kwa mchezaji mwenyewe, Coastal Union au Mgambo Shooting kama ulivunjwa au umenunulia na klabu anayotaka kuchezea msimu huu.
Tanzania Prisons inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji James Mjinja Magafu kutoka Toto Africans na Six Ally Mwasekaga (Majimaji). Nayo Coastal Union inatakiwa kumfanyia uhamisho mchezaji Kenneth Abeid Masumbuko kutoka Polisi Morogoro.
Kagera Sugar inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Suleiman Kibuta Rajab (Toto Africans), Godfrey Innocent Wambura (Abajalo), Eric Mulera Muliro (Toto Africans), Adam Juma Kingwande (African Lyon) na Peter Gideon Mutabuzi (Toto Africans).
Pia Kagera Sugar imepata Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya mchezaji Kitagenda Hamis Bukenya, lakini bado hana kibali cha kufanyia kazi nchini (work permit).
Kwa upande wa Ruvu Shooting inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Abdul Juma Seif (African Lyon), Lambele Jerome Reuben (Ashanti United), Juma Seif Dion (African Lyon) na Cosmas Ader Lewis (African Lyon).
 Oljoro JKT inatakiwa kumfanyia uhamisho mchezaji Tizzo Charles Chomba kutoka Polisi Morogoro, lakini imekataliwa kumsajili mchezaji Damas Mussa Kugesha wa Mlale JKT kwa kigezo kuwa ni askari na amehamishiwa Arusha kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi. Kama Oljoro JKT inamtaka mchezaji huyo ni lazima ifuate taratibu za usajili kwa kumfanyia uhamisho kutoka Mlale JKT.
 Nayo Mtibwa Sugar inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Ally Shomari Sharrif (Polisi Morogoro), Salim Hassan Mbonde (Oljoro JKT U20) na Hassan Salum Mbande iliyemsajili kwenye kikosi chake cha U20 akitokea Oljoro JKT U20.
Ashanti United haiwezi kumtumia Said Maulid Kalikula aliyekuwa akicheza Angola kwa vile hajapata ITC. Nayo Rhino Rangers inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Ally Ahmad Mwanyiro (Mwadui FC), Laban David Kambole (Toto Africans) na Musa Boaz Chibwabwa (Villa Squad).
Klabu ya Simba inatakiwa kumfanyia uhamisho Betram Arcadi Mwombeki kutoka Pamba SC wakati wachezaji Gilbert John Kaze na Amisi Tambwe bado hawajapata ITC kutoka Burundi na hawana vibali vya kufanya kazi nchini. Mchezaji Joseph Owino tayari ITC imepatikana lakini hana kibali cha kufanya kazi nchini. Pia kipa Abel right Dhaila hana kibali cha kufanya kazi nchini.
 Vilevile Simba inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji wawili iliyowasajili katika kikosi chake cha U20. Wachezaji hao ni Twaha Shekue Ibrahim kutoka Coastal Union 20 na Adeyun Saleh Seif (Oljoro JKT U20).
Nayo Yanga inatakiwa kumfanyia uhamisho mchezaji Rajabu Zahir Mohamed kutoka Mtibwa Sugar U20 wakati Hussein Omari Javu bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Mtibwa Sugar huku kukiwa hakuna vielelezo vyovyote kutoka kwa mchezaji mwenyewe, Mtibwa Sugar au Yanga kama mkataba huo ulivunjwa au umenunulia na klabu anayotaka kuchezea msimu huu.
 Wachezaji waliosajiliwa kutoka nje ambao ITC zimefika na pia wana vibali vya kufanya kazi nchini ni Crispine Odula Wadenya kutoka Bandari ya Kenya na Yayo Wasajja Fred Lutimba kutoka URA ya Uganda waliojiunga na timu ya Coastal Union. Pia Mtanzania Hamis Thabit Nyige aliyejiunga na Yanga kutoka Ureno naye tayari na ITC.
Kwa mujibu wa kanuni, wachezaji wote wa ridhaa (wa madaraja ya chini ikiwemo Daraja la Kwanza) wanatakiwa kufanyiwa uhamisho (transfer) kwa klabu husika kujaza fomu za uhamisho na kulipia ada Chama cha Mpira wa Miguu cha Wilaya, Chama cha Mpira wa Miguu cha Mkoa na TFF.
Pia TFF inakumbusha kuwa wachezaji wanaotajwa kuwa wamesajiliwa kama wachezaji huru (free agent) ni lazima waoneshwe kama huko walipokuwa mikataba imekwisha au la.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)


Jumatano, 21 Agosti 2013

Muumini 'Kocha wa Dunia' na Waziri Sonyo wa Victoria Sound, wazichapa kavukavu

Wanamuziki wawili nguli, Waziri Sonyo na Muumin Mwinjuma 'kocha wa Dunia', Rais aliyevuliwa uongozi wa bendi ya Victoria Sound, juzi wamezichapa kavu kavu wakati wa  mazoezi ya bendi yao yaliyofanyika Mbagala, jijini Dar es Salaam.
 
Katika kichapo hicho, inadaiwa kuwa Sonyo nusura amchome Muumini kisu, hivyo kuzua hofu katika patashika hilo la aina yake linaloendelea kuonyesha mgogoro mkubwa kati ya wanamuziki hao ndani ya bendi ya Victoria Sound.

Akizungumza muda mchache baada ya sakata hilo, Muumini alisema alishangaa kujikuta yupo chini na Sonyo akiwa ameshatoa kisu kutaka kumjeruhi.

Muda mchache baadaye Muumini aliandika kwenye mtandao wa kijamii akielezea tukio hilo alilodai ni la aina yake huku akitumia lugha kali za kuudhi dhidi ya Sonyo.
“Leo ndio nimedhihirisha huyu (TUSI LIMEHIFADHIWA) ni kweli amenikuta nimekaa tena pembeni na tahadhali zote ila alivyokuja kwangu kunivamia sikumkawiza nikampa ngumi 3 takatifu zilizolenga uso wake ndio akaona kumbe huyu mzima akatoa kisu mfuko wa kulia watu wakamuwahi kumshika, lakini wakati nakwepa kisu nilianguka, na kama sio George Gama angekuwa ameshanijeruhi au kuniua kabisa, ngoja nimfunze adabu nampeleka mahakamani ili iwe fundisho na kwa hili sina msalie mtume hivi jimwili lote la Sonyo Bado anamshikia mwanaume mwenzie Kisu na amshukuru, Janurry aliyenipakata ningempukutisha meno kwa ngumi maana alikuwa kama kuku mgonjwa hakurusha hata ngumi," mwisho wa kunukuu meseji ya Muumini.
Kupigana kwa wanamuziki hao ni mwendelezo wa mgogoro mzito uliokuwapo kwa bendi hiyo baada ya uongozi pia kumuondoa katika nafasi ya urais Muumini na kumpa Kassim Muhumba, huku pia Sonyo akienguliwa katika nafasi yake ya kiongozi wa shoo.

Je ni kweli Kocha wa dunia atajiweka pembeni na kuachana na muziki kama alivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari hivi karibuni, kama alivyoesema kuwa iwapo Victoria Sound itakufa ama kuondoka katika bendi hiyo, basi ataachana na muziki na matukio haya inawezekana mwanamuziki huyo ameanza kujilaumu kwa kauli hizo TATA.
Chanzo:- Lenzi ya Michezo

Jumanne, 20 Agosti 2013

UBAGUZI WAIPONZA LAZIO KUCHEZA BILA MASHABIKI

Mchezo wa Lazio

Lazio katika Serie A
Katika michezo sehemu ya uwanja wa klabu ya Lazio ya Italia imefungwa kwa mechi moja pekee kufuatia mashabiki kuwatusi wachezaji weusi.
Wachezaji watatu wa Juve Mfaransa Paul Pogba, Kwadwo Asamoah na Angelo Ogbonna kutoka Ghana na mchezaji wa Itali mwenye asili ya Nigeria walirushiwa matusi na mashabiki kwenye uwanja wa Stadio Olimpiko mjini Roma.
Hii ina maana kwamba mechi ya kwanza baina ya Lazio na Udinese katika Ligi ya Serie A itafanyika bila mashabiki uwanjani.
Kwingine hata kwa klabu za Arsenal na Fenebahce michuano ya Ligi ya mabingwa Ulaya ni muhimu kutokana na mapato.
Jumatano hii Arsenal iliyozongwa na matatizo inapambana na klabu inayokabiliwa na kesi mahakamani ikitishiwa kuondolewa mashindanoni.
Mawakili wa Fehnebahce wanaanza kusikiliza kesi kwa siku mbili huko Uswizi kuhusu tuhuma za ubadhirifu.
Shirikisho la UEFA liliruhusu klabu hio ishiriki mechi mbili dhidi ya Arsenal ingawa matokeo ya mahakama yanaweza yakaiondolea ushindi hata ikiwa imeshinda mechi ya nyumbani na marudiano mjini London.
Huko India maofisa wa michezo wanatokwa jasho kwa wanariadha wao kukataliwa kushiriki michezo ya Bara Asia kwa sababu ya umri wao uliozidi ule unaoruhusiwa.
Wanariadha 17 wa India wakiwa sehemu ya kikosi cha watu 27 wa India walipatikana kua na zaidi ya miaka 17 inayotakiwa kwenye mashindano haya.

Jumatatu, 19 Agosti 2013

TWIGA STARS U20 MOJA KWA MOJA KOMBE LA DUNIA RAUNDI YA KWANZA


TIMU ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania ya umri chini ya miaka 20 inaanzia moja kwa moja raundi ya kwanza Kanda ya Afrika kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Canada.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa jana (Agosti 18 mwaka huu) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Tanzania imepangiwa kucheza na Msumbiji ambapo mechi ya kwanza itachezwa Dar es Salaam kati ya Oktoba 25, 26 au 27 mwaka huu.

Mechi ya marudiano itachezwa wiki mbili baadaye nchini Msumbiji. Mechi hiyo inatakiwa kuchezwa kati ya Novemba 8,9 au 10 mwaka huu. Iwapo itafanikiwa kuitoa Msumbiji itacheza raundi ya pili na mshindi wa mechi kati ya Botswana na Afrika Kusini.

Raundi ya Tatu ambayo ndiyo ya mwisho, mechi zake za kwanza zitachezwa kati ya Januari 10, 11 au 12 mwakani wakati zile za marudiano zitakuwa kati ya Januari 24,25 au 26 mwakani.

Sudan Kusini na Uganda ndizo timu pekee kwa Kanda ya Afrika zinazoanzia raundi ya mchujo ambapo katika mechi ya kwanza zitapambana kati ya Septemba 13,14 au 15 mwaka huu na kurudiana kati ya Septemba 27, 28 au 29 mwaka huu.

Nchi 17 za Afrika zimeingia kwenye michuano hiyo. Nchi hizo ni Afrika Kusini, Botswana, Burkina Faso, Equatorial Guinea, Ghana, Guinea Bissau, Ivory Coast, Misri, Morocco, Msumbiji, Namibia, Nigeria, Sudan Kusini, Tanzania, Tunisia, Uganda na Zambia.

Jumamosi, 17 Agosti 2013

Shushu 'atekwa' kwa muda msikiti wa Mtambani akipiga picha







Baadhi ya waumini wa Kiislamu Msikiti wa Mtambani wakiwa wamemzunguka askari Polisi, Jonathan Tossi (katikati aliyeshika kamera) wakimuhoji baada ya kumshikilia kwa muda, hata hivyo walimuachia kwa masharti ya kumtaka afute picha zote alizopiga eneo hilo.

Askari Polisi wakizunguka doria eneo la Msikiti wa Mtambani jijini Dar es Salaam kuhakikisha kuna amani.

Askari wa Jeshi la Polisi, Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakizunguka kufanya doria maeneo mbalimbali ya jijini la Dar es Salaam kuhakikisha kuna amani. (Picha kwa hisani ya Gazeti la Jambo Leo.)
 
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BAADHI ya waumini wa Kiislamu Msikiti wa Mtambani Jijini Dar es Salaam jana wamemkamata mmoja wa askari wa Jeshi la Polisi na kumshikilia kwa muda kabla ya kumwachia kwa masharti kadhaa. 
Kwa mujibu wa chanzo cha habari hizi kimebainisha askari aliyekamatwa ni Jonathan Tossi ambaye anafanya kazi kitengo cha habari na uhusiano wa Jeshi la Polisi.
Askari huyo alijikuta akiingia kwenye mikono ya waumini hao alipokuwa akitekeleza majukumu yake (kazini) akipiga picha mtaani maeneo ya Msikiti wa Mtambani jijini Dar es Salaam. Taarifa zaidi zinasema baada ya waumini hao kumkamata askari huyo walimuhoji kwa muda kisha kutaka kitambulisho chake na kumuamuru afute picha zote alizokuwa akipiga eneo hilo ili wamuachilie kwa usalama wake.
“Kutokana na kuhofia usalama wake alikubaliana nao na kisha kufuta picha zote alizopiga. Walimtaka pia aoneshe kitambulisho na kuhoji ni kwanini anapiga picha wakati yeye ni askari…baada ya kukubaliana na masharti hayo walimuachia,” kilisema chanzo chetu.
“Sisi wenyewe tunashangaa wapiga picha walikuwa wengi wa vyombo mbalimbali vya habari hatujui hawa walijuaje kwamba yule jamaa alikuwa askari na wakati alikuwa amevaa kiraia,” alisema shuhuda mmoja aliyekuwa eneo la tukio.
Jana mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ulinzi na doria iliimarishwa na Jeshi la Polisi ambapo magari na pikipiki za Polisi zikiwa na askari waliojiandaa kutuliza ghasia yalikuwa yakizunguka ikiwa ni kujiandaa kwa kukabiliana na vurugu zozote.
Mitaa kadhaa mwandishi wa mtandao huu alishuhudia askari walio na mabomu ya machozi, huku wakiwa wamevalia vifaa maalumu vya kujikinga na risasi wakizunguka kwenye magari yao maeneo mbalimbali likiwemo eneo la Msikiti wa Mtambani Kinondoni jijini Da rs Salaam, Msikiti wa Mwenge na mingine inayotajwa kama ya wanaharakati. 
Hata hivyo hakuna taarifa za kutokea vurugu zozote.
Taarifa ambazo hazikuthibitishwa zinasema doria ya polisi ililazimika kufanywa baada za kuwepo na taarifa kuwa huenda wafuasi wa Shekhe Issa Ponda wangelifanya fujo kutokana na kutoridhishwa na hatua ya kukamatwa kwa kiongozi huyo kwa tuhuma kadhaa zinazomkabili.
Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, kuzungumzia kwa kina taarifa hizi hazikuzaa matuna. 

thehabari.com