Wanamuziki wawili nguli, Waziri
Sonyo na Muumin Mwinjuma 'kocha wa Dunia', Rais aliyevuliwa uongozi wa bendi ya Victoria Sound,
juzi wamezichapa kavu kavu wakati wa mazoezi ya bendi yao yaliyofanyika
Mbagala, jijini Dar es Salaam.
Katika kichapo hicho, inadaiwa kuwa Sonyo
nusura amchome Muumini kisu, hivyo kuzua hofu katika patashika hilo la
aina yake linaloendelea kuonyesha mgogoro mkubwa kati ya wanamuziki hao
ndani ya bendi ya Victoria Sound.
Akizungumza muda mchache baada ya
sakata hilo, Muumini alisema alishangaa kujikuta yupo chini na Sonyo
akiwa ameshatoa kisu kutaka kumjeruhi.
Muda
mchache baadaye Muumini aliandika kwenye mtandao wa kijamii akielezea
tukio hilo alilodai ni la aina yake huku akitumia lugha kali za kuudhi
dhidi ya Sonyo.
“Leo ndio
nimedhihirisha huyu (TUSI LIMEHIFADHIWA) ni kweli amenikuta nimekaa tena
pembeni na tahadhali zote ila alivyokuja kwangu kunivamia sikumkawiza
nikampa ngumi 3 takatifu zilizolenga uso wake ndio akaona kumbe huyu
mzima akatoa kisu mfuko wa kulia watu wakamuwahi kumshika,
lakini wakati nakwepa kisu nilianguka, na kama sio George Gama angekuwa
ameshanijeruhi au kuniua kabisa, ngoja nimfunze adabu nampeleka
mahakamani ili iwe fundisho na kwa hili sina msalie mtume hivi jimwili
lote la Sonyo Bado anamshikia mwanaume mwenzie Kisu na amshukuru,
Janurry aliyenipakata ningempukutisha meno kwa ngumi maana alikuwa kama
kuku mgonjwa hakurusha hata ngumi," mwisho wa kunukuu meseji ya Muumini.
Kupigana kwa
wanamuziki hao ni mwendelezo wa mgogoro mzito uliokuwapo kwa bendi hiyo
baada ya uongozi pia kumuondoa katika nafasi ya urais Muumini na kumpa
Kassim Muhumba, huku pia Sonyo akienguliwa katika nafasi yake ya
kiongozi wa shoo.
Je
ni kweli Kocha wa dunia atajiweka pembeni na kuachana na muziki kama
alivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari hivi karibuni, kama
alivyoesema kuwa iwapo Victoria Sound itakufa ama kuondoka katika bendi
hiyo, basi ataachana na muziki na matukio haya inawezekana mwanamuziki
huyo ameanza kujilaumu kwa kauli hizo TATA.
Chanzo:- Lenzi ya Michezo