Kamati
ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
imezuia usajili wa wachezaji 37 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kutokana
na usajili wao kuwa na kasoro.
Klabu
husika zimetakiwa kurekebisha kasoro hizo kabla ya kuanza kuwatumia wachezaji
hao kwenye mechi za VPL ambazo zinaanza leo (Agosti 24 mwaka huu) katika
viwanja mbalimbali nchini.
JKT
Ruvu Stars inatakiwa kuwafanyia uhamisho (transfer) wachezaji Salum Machaku
Salum aliyekuwa Polisi Morogoro na Emmanuel Leonard Swita (Toto Africans).
Mgambo Shooting inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Mohamed Hussein Neto
(Toto Africans), Kulwa Said Manzi (Polisi Morogoro) na Mohamed Ally Samata
(African Lyon).
Pia
Salum Aziz Gilla anaonekana bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Coastal Union
huku kukiwa hakuna vielelezo vyovyote kutoka kwa mchezaji mwenyewe, Coastal
Union au Mgambo Shooting kama ulivunjwa au umenunulia na klabu anayotaka
kuchezea msimu huu.
Tanzania
Prisons inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji James Mjinja Magafu kutoka Toto
Africans na Six Ally Mwasekaga (Majimaji). Nayo Coastal Union inatakiwa
kumfanyia uhamisho mchezaji Kenneth Abeid Masumbuko kutoka Polisi Morogoro.
Kagera
Sugar inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Suleiman Kibuta Rajab (Toto
Africans), Godfrey Innocent Wambura (Abajalo), Eric Mulera Muliro (Toto
Africans), Adam Juma Kingwande (African Lyon) na Peter Gideon Mutabuzi (Toto
Africans).
Pia
Kagera Sugar imepata Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya mchezaji
Kitagenda Hamis Bukenya, lakini bado hana kibali cha kufanyia kazi nchini (work
permit).
Kwa
upande wa Ruvu Shooting inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Abdul Juma Seif
(African Lyon), Lambele Jerome Reuben (Ashanti United), Juma Seif Dion (African
Lyon) na Cosmas Ader Lewis (African Lyon).
Oljoro
JKT inatakiwa kumfanyia uhamisho mchezaji Tizzo Charles Chomba kutoka Polisi
Morogoro, lakini imekataliwa kumsajili mchezaji Damas Mussa Kugesha wa Mlale
JKT kwa kigezo kuwa ni askari na amehamishiwa Arusha kwa ajili ya mafunzo ya
kijeshi. Kama Oljoro JKT inamtaka mchezaji huyo ni lazima ifuate taratibu za
usajili kwa kumfanyia uhamisho kutoka Mlale JKT.
Nayo
Mtibwa Sugar inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Ally Shomari Sharrif
(Polisi Morogoro), Salim Hassan Mbonde (Oljoro JKT U20) na Hassan Salum Mbande
iliyemsajili kwenye kikosi chake cha U20 akitokea Oljoro JKT U20.
Ashanti
United haiwezi kumtumia Said Maulid Kalikula aliyekuwa akicheza Angola kwa vile
hajapata ITC. Nayo Rhino Rangers inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Ally
Ahmad Mwanyiro (Mwadui FC), Laban David Kambole (Toto Africans) na Musa Boaz
Chibwabwa (Villa Squad).
Klabu ya Simba inatakiwa kumfanyia
uhamisho Betram Arcadi Mwombeki kutoka Pamba SC wakati wachezaji Gilbert John
Kaze na Amisi Tambwe bado hawajapata ITC kutoka Burundi na hawana vibali vya
kufanya kazi nchini. Mchezaji Joseph Owino tayari ITC imepatikana lakini hana
kibali cha kufanya kazi nchini. Pia kipa Abel right Dhaila hana kibali cha
kufanya kazi nchini.
Vilevile
Simba inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji wawili iliyowasajili katika
kikosi chake cha U20. Wachezaji hao ni Twaha Shekue Ibrahim kutoka Coastal
Union 20 na Adeyun Saleh Seif (Oljoro JKT U20).
Nayo
Yanga inatakiwa kumfanyia uhamisho mchezaji Rajabu Zahir Mohamed kutoka Mtibwa
Sugar U20 wakati Hussein Omari Javu bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Mtibwa
Sugar huku kukiwa hakuna vielelezo vyovyote kutoka kwa mchezaji mwenyewe,
Mtibwa Sugar au Yanga kama mkataba huo ulivunjwa au umenunulia na klabu
anayotaka kuchezea msimu huu.
Wachezaji
waliosajiliwa kutoka nje ambao ITC zimefika na pia wana vibali vya kufanya kazi
nchini ni Crispine Odula Wadenya kutoka Bandari ya Kenya na Yayo Wasajja Fred
Lutimba kutoka URA ya Uganda waliojiunga na timu ya Coastal Union. Pia
Mtanzania Hamis Thabit Nyige aliyejiunga na Yanga kutoka Ureno naye tayari na
ITC.
Kwa
mujibu wa kanuni, wachezaji wote wa ridhaa (wa madaraja ya chini ikiwemo Daraja
la Kwanza) wanatakiwa kufanyiwa uhamisho (transfer) kwa klabu husika kujaza
fomu za uhamisho na kulipia ada Chama cha Mpira wa Miguu cha Wilaya, Chama cha
Mpira wa Miguu cha Mkoa na TFF.
Pia
TFF inakumbusha kuwa wachezaji wanaotajwa kuwa wamesajiliwa kama wachezaji huru
(free agent) ni lazima waoneshwe kama huko walipokuwa mikataba imekwisha au la.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)