http://www.mkcomputertweaks.com/mkgroup/fkbmksb.gifMatangazo

Tangaza nasi: mkatedaniel@gmail.com, +255 7666-00 69 70, +255 655-00 69 71, +255 787- 249594

Usilikose kila Jumapili

Jumatatu, 26 Agosti 2013

Goma Mashariki mwa Congo 'Kimenuka' tena


Raia wakibeba mwili wa mtu aliyeuawa Goma
 
Mapigano mapya yamezuka mwishoni mwa juma katika eneo la Goma, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo ripoti zinasema watu watatu walifariki baada ya makombora kurushwa katika maeneo ya makaazi ya watu.
Haijulikani ni nani aliyerusha makombora hayo lakini wanainchi wameandamana wakililaumu jeshi la kulinda amani la Umoja wa Mataifa MONUSCO kwa kile wanachodai limewashambulia waasi katika juhudi za kuwatimua kwenye eneo hilo.
Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wamewalaumu waasi kwa kurusha makombora hayo lakini hakuna kundi lolote la waasi ambalo limedai kuhusika na shambulio hilo.
Afrika Kusini, ambayo imechangia kikosi hicho cha kulinda amani, imekiri kuwa mwanajeshi wake mmoja amejeruhiwa katika mlipuko huo wa bomu.
Akizungumza kwa simu na BBC, Msemaji wa jeshi la Afrika Kusini, Brigedia Generali Kolani Mabanga, amesema mwanajeshi wake mmoja alijeruhiwa vibaya na kwa sasa anaendelea kupata matibabu huku mipango ya kumrejesha nyumbani kwa matibabu zaidi ikiendelea.
Hali ya ulinzi imeimarisha katika eneo hilo lakini wakaazi wa mji huo na viunga vyake wanasema hali bado ni ya wasi wasi.

source; bbc

Jumamosi, 24 Agosti 2013

DHAIRA, OWINO, KAZE, TAMBWE WAKWAMA SIMBA KUCHEZEA VPL


Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imezuia usajili wa wachezaji 37 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kutokana na usajili wao kuwa na kasoro.
 Klabu husika zimetakiwa kurekebisha kasoro hizo kabla ya kuanza kuwatumia wachezaji hao kwenye mechi za VPL ambazo zinaanza leo (Agosti 24 mwaka huu) katika viwanja mbalimbali nchini.
 JKT Ruvu Stars inatakiwa kuwafanyia uhamisho (transfer) wachezaji Salum Machaku Salum aliyekuwa Polisi Morogoro na Emmanuel Leonard Swita (Toto Africans). Mgambo Shooting inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Mohamed Hussein Neto (Toto Africans), Kulwa Said Manzi (Polisi Morogoro) na Mohamed Ally Samata (African Lyon).
 Pia Salum Aziz Gilla anaonekana bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Coastal Union huku kukiwa hakuna vielelezo vyovyote kutoka kwa mchezaji mwenyewe, Coastal Union au Mgambo Shooting kama ulivunjwa au umenunulia na klabu anayotaka kuchezea msimu huu.
Tanzania Prisons inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji James Mjinja Magafu kutoka Toto Africans na Six Ally Mwasekaga (Majimaji). Nayo Coastal Union inatakiwa kumfanyia uhamisho mchezaji Kenneth Abeid Masumbuko kutoka Polisi Morogoro.
Kagera Sugar inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Suleiman Kibuta Rajab (Toto Africans), Godfrey Innocent Wambura (Abajalo), Eric Mulera Muliro (Toto Africans), Adam Juma Kingwande (African Lyon) na Peter Gideon Mutabuzi (Toto Africans).
Pia Kagera Sugar imepata Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa ajili ya mchezaji Kitagenda Hamis Bukenya, lakini bado hana kibali cha kufanyia kazi nchini (work permit).
Kwa upande wa Ruvu Shooting inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Abdul Juma Seif (African Lyon), Lambele Jerome Reuben (Ashanti United), Juma Seif Dion (African Lyon) na Cosmas Ader Lewis (African Lyon).
 Oljoro JKT inatakiwa kumfanyia uhamisho mchezaji Tizzo Charles Chomba kutoka Polisi Morogoro, lakini imekataliwa kumsajili mchezaji Damas Mussa Kugesha wa Mlale JKT kwa kigezo kuwa ni askari na amehamishiwa Arusha kwa ajili ya mafunzo ya kijeshi. Kama Oljoro JKT inamtaka mchezaji huyo ni lazima ifuate taratibu za usajili kwa kumfanyia uhamisho kutoka Mlale JKT.
 Nayo Mtibwa Sugar inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Ally Shomari Sharrif (Polisi Morogoro), Salim Hassan Mbonde (Oljoro JKT U20) na Hassan Salum Mbande iliyemsajili kwenye kikosi chake cha U20 akitokea Oljoro JKT U20.
Ashanti United haiwezi kumtumia Said Maulid Kalikula aliyekuwa akicheza Angola kwa vile hajapata ITC. Nayo Rhino Rangers inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji Ally Ahmad Mwanyiro (Mwadui FC), Laban David Kambole (Toto Africans) na Musa Boaz Chibwabwa (Villa Squad).
Klabu ya Simba inatakiwa kumfanyia uhamisho Betram Arcadi Mwombeki kutoka Pamba SC wakati wachezaji Gilbert John Kaze na Amisi Tambwe bado hawajapata ITC kutoka Burundi na hawana vibali vya kufanya kazi nchini. Mchezaji Joseph Owino tayari ITC imepatikana lakini hana kibali cha kufanya kazi nchini. Pia kipa Abel right Dhaila hana kibali cha kufanya kazi nchini.
 Vilevile Simba inatakiwa kuwafanyia uhamisho wachezaji wawili iliyowasajili katika kikosi chake cha U20. Wachezaji hao ni Twaha Shekue Ibrahim kutoka Coastal Union 20 na Adeyun Saleh Seif (Oljoro JKT U20).
Nayo Yanga inatakiwa kumfanyia uhamisho mchezaji Rajabu Zahir Mohamed kutoka Mtibwa Sugar U20 wakati Hussein Omari Javu bado ana mkataba wa mwaka mmoja na Mtibwa Sugar huku kukiwa hakuna vielelezo vyovyote kutoka kwa mchezaji mwenyewe, Mtibwa Sugar au Yanga kama mkataba huo ulivunjwa au umenunulia na klabu anayotaka kuchezea msimu huu.
 Wachezaji waliosajiliwa kutoka nje ambao ITC zimefika na pia wana vibali vya kufanya kazi nchini ni Crispine Odula Wadenya kutoka Bandari ya Kenya na Yayo Wasajja Fred Lutimba kutoka URA ya Uganda waliojiunga na timu ya Coastal Union. Pia Mtanzania Hamis Thabit Nyige aliyejiunga na Yanga kutoka Ureno naye tayari na ITC.
Kwa mujibu wa kanuni, wachezaji wote wa ridhaa (wa madaraja ya chini ikiwemo Daraja la Kwanza) wanatakiwa kufanyiwa uhamisho (transfer) kwa klabu husika kujaza fomu za uhamisho na kulipia ada Chama cha Mpira wa Miguu cha Wilaya, Chama cha Mpira wa Miguu cha Mkoa na TFF.
Pia TFF inakumbusha kuwa wachezaji wanaotajwa kuwa wamesajiliwa kama wachezaji huru (free agent) ni lazima waoneshwe kama huko walipokuwa mikataba imekwisha au la.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)


Jumatano, 21 Agosti 2013

Muumini 'Kocha wa Dunia' na Waziri Sonyo wa Victoria Sound, wazichapa kavukavu

Wanamuziki wawili nguli, Waziri Sonyo na Muumin Mwinjuma 'kocha wa Dunia', Rais aliyevuliwa uongozi wa bendi ya Victoria Sound, juzi wamezichapa kavu kavu wakati wa  mazoezi ya bendi yao yaliyofanyika Mbagala, jijini Dar es Salaam.
 
Katika kichapo hicho, inadaiwa kuwa Sonyo nusura amchome Muumini kisu, hivyo kuzua hofu katika patashika hilo la aina yake linaloendelea kuonyesha mgogoro mkubwa kati ya wanamuziki hao ndani ya bendi ya Victoria Sound.

Akizungumza muda mchache baada ya sakata hilo, Muumini alisema alishangaa kujikuta yupo chini na Sonyo akiwa ameshatoa kisu kutaka kumjeruhi.

Muda mchache baadaye Muumini aliandika kwenye mtandao wa kijamii akielezea tukio hilo alilodai ni la aina yake huku akitumia lugha kali za kuudhi dhidi ya Sonyo.
“Leo ndio nimedhihirisha huyu (TUSI LIMEHIFADHIWA) ni kweli amenikuta nimekaa tena pembeni na tahadhali zote ila alivyokuja kwangu kunivamia sikumkawiza nikampa ngumi 3 takatifu zilizolenga uso wake ndio akaona kumbe huyu mzima akatoa kisu mfuko wa kulia watu wakamuwahi kumshika, lakini wakati nakwepa kisu nilianguka, na kama sio George Gama angekuwa ameshanijeruhi au kuniua kabisa, ngoja nimfunze adabu nampeleka mahakamani ili iwe fundisho na kwa hili sina msalie mtume hivi jimwili lote la Sonyo Bado anamshikia mwanaume mwenzie Kisu na amshukuru, Janurry aliyenipakata ningempukutisha meno kwa ngumi maana alikuwa kama kuku mgonjwa hakurusha hata ngumi," mwisho wa kunukuu meseji ya Muumini.
Kupigana kwa wanamuziki hao ni mwendelezo wa mgogoro mzito uliokuwapo kwa bendi hiyo baada ya uongozi pia kumuondoa katika nafasi ya urais Muumini na kumpa Kassim Muhumba, huku pia Sonyo akienguliwa katika nafasi yake ya kiongozi wa shoo.

Je ni kweli Kocha wa dunia atajiweka pembeni na kuachana na muziki kama alivyonukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari hivi karibuni, kama alivyoesema kuwa iwapo Victoria Sound itakufa ama kuondoka katika bendi hiyo, basi ataachana na muziki na matukio haya inawezekana mwanamuziki huyo ameanza kujilaumu kwa kauli hizo TATA.
Chanzo:- Lenzi ya Michezo

Jumanne, 20 Agosti 2013

UBAGUZI WAIPONZA LAZIO KUCHEZA BILA MASHABIKI

Mchezo wa Lazio

Lazio katika Serie A
Katika michezo sehemu ya uwanja wa klabu ya Lazio ya Italia imefungwa kwa mechi moja pekee kufuatia mashabiki kuwatusi wachezaji weusi.
Wachezaji watatu wa Juve Mfaransa Paul Pogba, Kwadwo Asamoah na Angelo Ogbonna kutoka Ghana na mchezaji wa Itali mwenye asili ya Nigeria walirushiwa matusi na mashabiki kwenye uwanja wa Stadio Olimpiko mjini Roma.
Hii ina maana kwamba mechi ya kwanza baina ya Lazio na Udinese katika Ligi ya Serie A itafanyika bila mashabiki uwanjani.
Kwingine hata kwa klabu za Arsenal na Fenebahce michuano ya Ligi ya mabingwa Ulaya ni muhimu kutokana na mapato.
Jumatano hii Arsenal iliyozongwa na matatizo inapambana na klabu inayokabiliwa na kesi mahakamani ikitishiwa kuondolewa mashindanoni.
Mawakili wa Fehnebahce wanaanza kusikiliza kesi kwa siku mbili huko Uswizi kuhusu tuhuma za ubadhirifu.
Shirikisho la UEFA liliruhusu klabu hio ishiriki mechi mbili dhidi ya Arsenal ingawa matokeo ya mahakama yanaweza yakaiondolea ushindi hata ikiwa imeshinda mechi ya nyumbani na marudiano mjini London.
Huko India maofisa wa michezo wanatokwa jasho kwa wanariadha wao kukataliwa kushiriki michezo ya Bara Asia kwa sababu ya umri wao uliozidi ule unaoruhusiwa.
Wanariadha 17 wa India wakiwa sehemu ya kikosi cha watu 27 wa India walipatikana kua na zaidi ya miaka 17 inayotakiwa kwenye mashindano haya.

Jumatatu, 19 Agosti 2013

TWIGA STARS U20 MOJA KWA MOJA KOMBE LA DUNIA RAUNDI YA KWANZA


TIMU ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania ya umri chini ya miaka 20 inaanzia moja kwa moja raundi ya kwanza Kanda ya Afrika kutafuta tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Canada.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa jana (Agosti 18 mwaka huu) na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Tanzania imepangiwa kucheza na Msumbiji ambapo mechi ya kwanza itachezwa Dar es Salaam kati ya Oktoba 25, 26 au 27 mwaka huu.

Mechi ya marudiano itachezwa wiki mbili baadaye nchini Msumbiji. Mechi hiyo inatakiwa kuchezwa kati ya Novemba 8,9 au 10 mwaka huu. Iwapo itafanikiwa kuitoa Msumbiji itacheza raundi ya pili na mshindi wa mechi kati ya Botswana na Afrika Kusini.

Raundi ya Tatu ambayo ndiyo ya mwisho, mechi zake za kwanza zitachezwa kati ya Januari 10, 11 au 12 mwakani wakati zile za marudiano zitakuwa kati ya Januari 24,25 au 26 mwakani.

Sudan Kusini na Uganda ndizo timu pekee kwa Kanda ya Afrika zinazoanzia raundi ya mchujo ambapo katika mechi ya kwanza zitapambana kati ya Septemba 13,14 au 15 mwaka huu na kurudiana kati ya Septemba 27, 28 au 29 mwaka huu.

Nchi 17 za Afrika zimeingia kwenye michuano hiyo. Nchi hizo ni Afrika Kusini, Botswana, Burkina Faso, Equatorial Guinea, Ghana, Guinea Bissau, Ivory Coast, Misri, Morocco, Msumbiji, Namibia, Nigeria, Sudan Kusini, Tanzania, Tunisia, Uganda na Zambia.

Jumamosi, 17 Agosti 2013

Shushu 'atekwa' kwa muda msikiti wa Mtambani akipiga picha







Baadhi ya waumini wa Kiislamu Msikiti wa Mtambani wakiwa wamemzunguka askari Polisi, Jonathan Tossi (katikati aliyeshika kamera) wakimuhoji baada ya kumshikilia kwa muda, hata hivyo walimuachia kwa masharti ya kumtaka afute picha zote alizopiga eneo hilo.

Askari Polisi wakizunguka doria eneo la Msikiti wa Mtambani jijini Dar es Salaam kuhakikisha kuna amani.

Askari wa Jeshi la Polisi, Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakizunguka kufanya doria maeneo mbalimbali ya jijini la Dar es Salaam kuhakikisha kuna amani. (Picha kwa hisani ya Gazeti la Jambo Leo.)
 
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
BAADHI ya waumini wa Kiislamu Msikiti wa Mtambani Jijini Dar es Salaam jana wamemkamata mmoja wa askari wa Jeshi la Polisi na kumshikilia kwa muda kabla ya kumwachia kwa masharti kadhaa. 
Kwa mujibu wa chanzo cha habari hizi kimebainisha askari aliyekamatwa ni Jonathan Tossi ambaye anafanya kazi kitengo cha habari na uhusiano wa Jeshi la Polisi.
Askari huyo alijikuta akiingia kwenye mikono ya waumini hao alipokuwa akitekeleza majukumu yake (kazini) akipiga picha mtaani maeneo ya Msikiti wa Mtambani jijini Dar es Salaam. Taarifa zaidi zinasema baada ya waumini hao kumkamata askari huyo walimuhoji kwa muda kisha kutaka kitambulisho chake na kumuamuru afute picha zote alizokuwa akipiga eneo hilo ili wamuachilie kwa usalama wake.
“Kutokana na kuhofia usalama wake alikubaliana nao na kisha kufuta picha zote alizopiga. Walimtaka pia aoneshe kitambulisho na kuhoji ni kwanini anapiga picha wakati yeye ni askari…baada ya kukubaliana na masharti hayo walimuachia,” kilisema chanzo chetu.
“Sisi wenyewe tunashangaa wapiga picha walikuwa wengi wa vyombo mbalimbali vya habari hatujui hawa walijuaje kwamba yule jamaa alikuwa askari na wakati alikuwa amevaa kiraia,” alisema shuhuda mmoja aliyekuwa eneo la tukio.
Jana mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam ulinzi na doria iliimarishwa na Jeshi la Polisi ambapo magari na pikipiki za Polisi zikiwa na askari waliojiandaa kutuliza ghasia yalikuwa yakizunguka ikiwa ni kujiandaa kwa kukabiliana na vurugu zozote.
Mitaa kadhaa mwandishi wa mtandao huu alishuhudia askari walio na mabomu ya machozi, huku wakiwa wamevalia vifaa maalumu vya kujikinga na risasi wakizunguka kwenye magari yao maeneo mbalimbali likiwemo eneo la Msikiti wa Mtambani Kinondoni jijini Da rs Salaam, Msikiti wa Mwenge na mingine inayotajwa kama ya wanaharakati. 
Hata hivyo hakuna taarifa za kutokea vurugu zozote.
Taarifa ambazo hazikuthibitishwa zinasema doria ya polisi ililazimika kufanywa baada za kuwepo na taarifa kuwa huenda wafuasi wa Shekhe Issa Ponda wangelifanya fujo kutokana na kutoridhishwa na hatua ya kukamatwa kwa kiongozi huyo kwa tuhuma kadhaa zinazomkabili.
Juhudi za kumpata Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, kuzungumzia kwa kina taarifa hizi hazikuzaa matuna. 

thehabari.com

UCHAGUZI TFF BAADA YA MECHI YA SIMBA NA YANGA





Boniface Wambura, Ofisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa kuzingatia mamlaka iliyonayo katika kifungu cha 10(6) cha Kanuni za Uchaguzi za TFF inasogeza mbele tarehe ya uchaguzi wa TFF kutoka Oktoba 20 mpaka Oktoba 26 na 27 mwaka huu.

Sababu za kusogeza mbele uchaguzi ni kutokana na ukweli kuwa Oktoba 20 mwaka huu uongozi wa TFF utakuwa na shughuli nyingi za maandalizi ya mechi ya Simba na Yanga, na hivyo haitawezekana kusimamia shughuli za Mkutano Mkuu wa Uchaguzi kwa wakati mmoja na mchezo huo.

Siku ya mwisho ya kampeni itakuwa Oktoba 25 mwaka huu. Ukiondoa  mabadiliko hayo ya tarehe ya uchaguzi wa viongozi wa TFF, ratiba ya mchakato wa uchaguzi na itabaki kama ilivyotangazwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF katika mkutano wake na waandishi wa habari Agosti 24 mwaka huu.

Pia Kamati imeamua kuwa uchaguzi wa Bodi ya Ligi utabakia kuwa Oktoba 18 mwaka huu kama ilivyopangwa awali.

Kamati imesema inaamini wahusika wote watapokea vizuri mabadiliko hayo na inasikitika kwa usumbufu utakaosababishwa na mabadiliko hayo.

Ijumaa, 16 Agosti 2013

Libya kushambulia kwa makombora meli za mafuta

 16 Agosti, 2013 - Saa 11:04 GMT
Kisima cha mafuta Libya
Waziri Mkuu wa Libya,Ali Zeidan ametishia kutumia nguvu kuwazuia walinzi katika bandari kuu nchini humo dhidi ya kuuza mafuta kwa mashirika ya kibinafsi.
Afisa huyo amesema meli yeyote itakayotia nanga katika bandari za Libya bila idhini ya serikali itashambuliwa kwa bomu.Wafanyakazi wa badari wamekua kwenye mgomo wiki kadhaa sasa kulalamikia malipo. Maafisa wamesema mgomo huo umesababisha kupungua kwa mauzo ya mafuta nchini Libya na hivyo kuathiri vibaya uchumi wa nchi.
Waziri Mkuu amesema serikali itatumia nguvu zozote zile kuzuia kile amesema kuvuruga biashara ya mafuta. Banadari zilizoathirika na mgomo ni pamoja na Zeitunia, Brega, Ras Lanouf na Sedra. Uzalishaji wa mafuta Libya ulipungua hadi mapipa laki sita kutoka mapipa milioni moja baada ya kuzuka mapinduzi dhidi ya kiongozi wa zamani Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011.

source: bbc

Jumamosi, 10 Agosti 2013

SHEHE PONDA AJERUHIWA NA POLISI MOROGORO

Habari zilizo tufikia hivi punde katika meza yetu ya habari ya Father Kidevu Blog, zinapasha kuwa Sheikh Ponda Issa Ponda anadaiwa kujeruhiwa na Polisi muda mfupi baada ya kumaliza mhadhara wake Mjini Morogoro katika jaribio la kumkamata.

Taarifa kutoka eeo la tukio zinapasha kuwa Sheikh Ponda amejeruhiwa na bomu la machozi lililoplipuliwa katika gari lake wakati wa jaribio hilo la kumkamata jioni ya leo na kuzua mtafaruku mkali.

Aidha taarifa hizo zinasema mara baada ya tukio hilo baadhi ya Mashekh walimshusha katika gari lake na kumpakia katika Pikipiki na kumkimbiza Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu lakini ghafla walibaini kuwa Polisi wanawafuatilia na kuamua kuingia hospitalini hapo na kutokea mlango wa uwani na kutokomea.


Mtoa taarifa wa Fadha Kidevu Blog mjini Mrogoro anapasha kuwa wakati Ponda akitoroshwa mikononi mwa Polisi mlango wa uwani Polisi walitinga Hospitalini humo kufanya msako wa Shekh huyo ambaye amekuwa akileta kizazaa zaa kutoka na mawaidha yake na msimamo wake wa utetezi wa mali za Waislamu nchini.
Father Kidevu Blog itakupa taarifa kamili ya tukio hilo wakati wowote kuanzia sasa endelea kuifuatilia.

ACP KOVA AKIZINDUA ALBAMU YA KASWIDA YA KUOMBEA AMANI NCHI VIWANJA VYA MNAZI MMOJA LEO

 1. Mtunzi wa albamu ya kaswida ya kundi la Swautun Naqy akitumbuiza leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja leo
 2. ACP Kova akiandika jambo huku Shehe wa Mkoa wa Dar, Alhaji Musa Salum akisikiliza kwa makini kaswida
3. ACP Kova akizungumza jambo katika uzinduzi wa albamu ya Kaswida leo Mnazi mmoja jijini Dar
 4.ACP Kova akiwa ameishikiria albamu huku Alhaji Musa akimwangalia
5. Kamanda Kova akiwa ameshikiria albamu na pesa Sh.50,000 taslimu alizonunulia albamu hiyo ya kaswida ya kuombea amani nchini.

BONDIA MIYEYUSHO 'AMYEYUSHA' MZAMBIA KWA KO RAUNDI YA 8


Bondia Mtanzania Francis Miyeyusho kulia  akipambana na Fidelis Lupupa wa Zambia wakati wa  mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika wakati wa Sikuku ya Iddi katika ukumbi wa Dar Live Mbagara Miyeyusho alishinda kwa K,O ya raundi ya nane 
Bondia Mtanzania Francis Miyeyusho kushoto  akipambana na Fidelis Lupupa wa Zambia wakati wa  mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika wakati wa Sikuku ya Iddi katika ukumbi wa Dar Live Mbagara Miyeyusho alishinda kwa K,O ya raundi ya nane pic
Bondia KaSIM rAJABU AKIPAMBANA NA kEVIN fABIAN WAKATI WA MPAMBANO WAKE ULIOFANYIKA SIKU YA SIKUKUU YA iDDI KATIKA UKUMBI WA dAR lIVE dAR ES SALAAM fABIAN ALISHINDA KWA pOINT
Bondia Godfrey Pancho kushoto akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Hamisi Mohamedi wakati wa mpambano wao uliofanyika sikukuu ya Iddi mosi katika ukumbi wa Dar Live Mbagara
Bondia Godfrey Pancho kulia akioneshana ufundi wa kutupiana makonde na Hamisi Mohamedi wakati wa mpambano wao uliofanyika sikukuu ya Iddi mosi katika ukumbi wa Dar Live Mbagara
Bondia Chipaki Chipindi akiwa na mashabiki wake baada ya kumkarisha raundi ya kwanza bondia Ramadhani Kido


Bondia Fidelis Lupupa wa Zambia akiwa chini amekaa akijifikilia kuwa aendelee au asienderee baada ya kupigwa na bondia Mtanzania Francis Miyeyusho wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagara Dar es salaam Miyeyusho alishinda kwa K,o ya raundi ya nane 
Bondia Mtanzania Francis Miyeyusho kulia  akipambana na Fidelis Lupupa wa Zambia wakati wa  mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika wakati wa Sikuku ya Iddi katika ukumbi wa Dar Live Mbagara Miyeyusho alishinda kwa K,O ya raundi ya nane 
Bondia Fidelis Lupupa wa Zambia akiwa chini amekaa akijifikilia kuwa aendelee au asienderee baada ya kupigwa na bondia Mtanzania Francis Miyeyusho wakati wa mpambano wao uliofanyika katika ukumbi wa Dar Live Mbagara Dar es salaam Miyeyusho alishinda kwa K,o ya raundi ya nane Picha zote na SUPER D
Bondia Mtanzania Francis Miyeyusho kushoto  akipambana na Fidelis Lupupa wa Zambia wakati wa  mpambano wao wa kirafiki wa kimataifa uliofanyika wakati wa Sikuku ya Iddi katika ukumbi wa Dar Live Mbagara Miyeyusho alishinda kwa K,O ya raundi ya nane 

MIYEYUSHO AKISHANGILIA USHINDI

MIYEYUSHO AKIWA KATIKA POZI

MAGOROFA YABOMOLEWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

MAGOROFA YABOMOLEWA JIJINI DAR ES SALAAM LEO
aSKARI POLISI WAKIWA KATIKA DORIA WAKATI WA UBOMOAJI WA MAGOROFA KATIKA BARABARA YA SAMORA LEO


ENEO LA MAGOROFA YANAYOBOMOLEWA KATIKATI YA MJI BARABARA YA SAMORA JIJINI DAR ES SALAAM MAGOROFA HAYO YALE AMBAYO YAMESHAKUWA MAGOFU LEO

Ijumaa, 9 Agosti 2013

Meya Mwenda awapa 'tiketi' wakazi waliokombolewa mashamba yao

1. Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda (kushoto) akisaini moja ya mikataba na wakazi waliokombolewa maeneo yao huko Madale, Nakasangwe, Nakalekwa, Kazaroho, Kinondo na Boko.
Katikati ni mwenyekiti wa wakazi hao waliokombolewa maeneo yao toka mikononi mwa wavamizi, Seif Maungu na kulia ni Afisa Utumishi wa Manispaa ya Kinondoni, Godfrey Mugumi aliyesaini kwa niaba ya mkurugenzi wa manispaa iyo, Mussa Natty.




2. Seif Maungu (kushoto) akisaini mkataba, huku katikati akiwa Afisa Utumishi wa Manispaa ya Kinondoni, Godfrey na kulia ni katibu wa wakazi hao waliokolewa maeneo yao, Kosta.
3. Wakazi waliookolewa maeneo yao wakiwa katika ofisi ya Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, wakimsikiliza mwenyekiti wao akiwasomea yaliyomo ndani ya mkataba waliowekeana na Manispaa hiyo