16 Agosti, 2013 - Saa 11:04 GMT
Waziri Mkuu wa Libya,Ali Zeidan
ametishia kutumia nguvu kuwazuia walinzi katika bandari kuu nchini humo
dhidi ya kuuza mafuta kwa mashirika ya kibinafsi.
Afisa huyo amesema meli yeyote itakayotia nanga
katika bandari za Libya bila idhini ya serikali itashambuliwa kwa
bomu.Wafanyakazi wa badari wamekua kwenye mgomo wiki kadhaa sasa
kulalamikia malipo. Maafisa wamesema mgomo huo umesababisha kupungua kwa
mauzo ya mafuta nchini Libya na hivyo kuathiri vibaya uchumi wa nchi.Waziri Mkuu amesema serikali itatumia nguvu zozote zile kuzuia kile amesema kuvuruga biashara ya mafuta. Banadari zilizoathirika na mgomo ni pamoja na Zeitunia, Brega, Ras Lanouf na Sedra. Uzalishaji wa mafuta Libya ulipungua hadi mapipa laki sita kutoka mapipa milioni moja baada ya kuzuka mapinduzi dhidi ya kiongozi wa zamani Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011.
source: bbc