Habari
zilizo tufikia hivi punde katika meza yetu ya habari ya Father Kidevu
Blog, zinapasha kuwa Sheikh Ponda Issa Ponda anadaiwa kujeruhiwa na
Polisi muda mfupi baada ya kumaliza mhadhara wake Mjini Morogoro katika
jaribio la kumkamata.
Taarifa
kutoka eeo la tukio zinapasha kuwa Sheikh Ponda amejeruhiwa na bomu la
machozi lililoplipuliwa katika gari lake wakati wa jaribio hilo la
kumkamata jioni ya leo na kuzua mtafaruku mkali.
Aidha
taarifa hizo zinasema mara baada ya tukio hilo baadhi ya Mashekh
walimshusha katika gari lake na kumpakia katika Pikipiki na kumkimbiza
Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kwa matibabu lakini ghafla walibaini kuwa
Polisi wanawafuatilia na kuamua kuingia hospitalini hapo na kutokea
mlango wa uwani na kutokomea.
Mtoa
taarifa wa Fadha Kidevu Blog mjini Mrogoro anapasha kuwa wakati Ponda
akitoroshwa mikononi mwa Polisi mlango wa uwani Polisi walitinga
Hospitalini humo kufanya msako wa Shekh huyo ambaye amekuwa akileta
kizazaa zaa kutoka na mawaidha yake na msimamo wake wa utetezi wa mali
za Waislamu nchini.
Father Kidevu Blog itakupa taarifa kamili ya tukio hilo wakati wowote kuanzia sasa endelea kuifuatilia.