http://www.mkcomputertweaks.com/mkgroup/fkbmksb.gifMatangazo

Tangaza nasi: mkatedaniel@gmail.com, +255 7666-00 69 70, +255 655-00 69 71, +255 787- 249594

Usilikose kila Jumapili

Jumamosi, 20 Aprili 2013

'Jeshi lawaua wauguzi' Sudan Kusini


 
Wauguzi watano wameuawa Sudan Kusini baada ya wanajeshi kushambulia hospitali moja kulipiza kisasi kwa mauaji ya wanajeshi wengine wanane.
Hii ni kwa mujibu wa mbunge mmoja wa eneo hilo.
David Mayo alisema kuwa makabiliano yangali yanaendelea na ameitaka serikali kuamuru jeshi kuondoka katika eneo hilo.
Viongozi wa kijamii wamethibitisha hospitali hiyo iliyoko katika jimbo la Eastern Equatorial ilishambuliwa ingawa taarifa kutoka ofisi ya gavana wa jimbo hilo imekanusha habari hizo.
Amesema kuwa jeshi lilikwenda pale kulinda raia.

Ufyatulianaji wa risasi kiholea.

Wanajeshi walipelekwa katika eneo hilo, baada ya walinzi wanane wa gavana wa jimbo hilo kuuawa walipotumwa kuwasaka wezi wa mifugo.
Mwandishi wa BBC wa masuala ya Sudan Kusini, Nyambura Wambugu anasema wakazi wengi wa eneo hilo lenye milima, wamejihami vikali wakiwa na maguruneti ambayo yalianguka mikononi mwao kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miongo miwili.
Mayo alisema kuwa wanajeshi 13 wanapatiwa matibabu mjini Torit.
Lakini amelaumu wanajeshi kwa mashambulizi hayo, akisema kuwa waliwafyatulia risasi watu kiholela walipowasili katika eneo la Lorema, kabla ya kushambulia hospitalini hiyo na kisha kuteketeza makazi ya watu.
Daktari mmoja, mgonjwa mmoja na wauguzi wanne waliuawa.

source: bbc

Ijumaa, 19 Aprili 2013

TAARIFA YA TFF- HERI AZAM

Release No. 068
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Aprili 19, 2013

KILA LA KHERI AZAM FC
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaitakia kila la kheri timu ya Azam FC katika mechi yake ya kwanza ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya AS FAR Rabat ya Morocco itakayochezwa kesho (Aprili 20 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

Azam FC ina fursa nzuri ya kufanya vizuri kwenye mechi hiyo itakayochezeshwa na mwamuzi Emile Fred kutoka Shelisheli kutokana na maandalizi iliyofanya, lakini vilevile tunatoa mwito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi uwanjani kuiunga mkono.

Makocha wasaidizi wa timu zote mbili, Kalimangonga Ongala wa Azam na Lahcen Ouadani wa AS FAR Rabat wamezungumza na waandishi wa habari kuhusu mechi hiyo, kuwa wamejiandaa kuibuka na ushindi.

Kocha Ongala amesema wamepata DVD za mechi tatu za mwisho za AS FAR Rabat, moja ikiwa dhidi ya timu ya Al Nasir ya Libya ambayo waliitoa katika raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho na nyingine mbili za ligi ya Morocco ambazo wanazifanyia kazi kuhakikisha wanashinda kesho.

Naye Ouadani amesema hawaifahamu vizuri Azam, lakini wanaujua mpira wa Tanzania baada ya kuangalia mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Morocco (Lions of the Atlas) iliyochezwa jijini Dar es Salaam Machi 24 mwaka huu na Stars kushinda mabao 3-1.

Baadhi ya wachezaji ambao Azam inatarajia kuwatumia kwenye mechi ya kesho ni pamoja na Aishi Manula, Mwadini Ally, Khamis Mcha, John Bocco na Salum Abubakar ambao pia wamo kwenye kikosi cha sasa cha Taifa Stars kilicho chini ya kocha Kim Poulsen.

AS FAR Rabat ina wachezaji sita kwenye timu ya Taifa ya Morocco. Wachezaji hao ni mabeki Younes Bellakhdar, Abderrahim Achchakir, Younnes Hammal, na viungo Salaheddine Said, Salaheddine Aqqal na Youssef Kaddioui.

LIGI YA MABINGWA WA MIKOA KUANZA MEI 12
Ligi ya Mabingwa wa Mikoa kutafuta timu tatu zitakazopanda kucheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu ujao chini ya usimamizi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) itaanza Mei 12 mwaka huu.

Mwisho wa mikoa kuwasilisha majina ya mabingwa wao ni Mei 1 mwaka huu wakati ratiba ya ligi hiyo itapangwa mbele ya waandishi wa habari Mei 3 mwaka huu kwenye ofisi za TFF.

Uwasilishaji wa jina la bingwa wa mkoa unatakiwa kufanyika pamoja na ulipaji ada ya ushiriki ambayo ni sh. 100,000. Mfumo wa ligi hiyo ni bingwa wa mkoa X kucheza na bingwa wa mkoa Y nyumbani na ugenini ambapo mshindi ndiye anayesonga mbele katika hatua inayofuata.

Usajili wa wachezaji wa timu hizo ni uleule uliofanyika katika hatua ya mkoa na unatakiwa kuwasilishwa TFF kwa ajili ya uthibitisho. TFF inapenda kusisitiza kuwa hakuna usajili mpya wa wachezaji kwa ajili ya ligi hiyo.


Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

TAARIFA TOKA OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI






JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI
 


TAARIFA KWA UMMA NA VYOMBO VYA HABARI

Ufafanuzi wa Taarifa Kuhusu Hali ya Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) zilizotolewa kwenye baadhi ya vyombo vya Habari siku ya Ijumaa tarehe 12 Aprili 2013 kutokana na ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliyotolewa Bungeni.

1.   UTANGULIZI
Siku ya Ijumaa ya tarehe 12 Aprili 2013 baadhi ya vyombo vya Habari viliandika juu ya taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali aliyoitoa Bungeni tarehe 11 Aprili, 2013 isivyo sahihi zinazohusu Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) kama ifuatavyo:
v  Kuwa Mfuko umepata hasara ya Shilingi trilioni 6.487 na hali yake kifedha ni mbaya.

v  Mfuko umekuwa ukitoa mikopo bila ya kutoza riba.

2.   UFAFANUZI
v  Kuwa Mfuko umepata hasara ya Shilingi trilioni 6.487 na hali yake kifedha ni mbaya.

Ninapenda kufafanua kuwa taarifa yangu ilivyotafsiriwa na baadhi ya vyombo vya habari kuwa Mfuko umepata hasara ya shilingi trilioni  6.487 siyo sahihi.


Taarifa sahihi ni kuwa kiasi hicho ni nakisi (acturial deficit) ambayo imetokana na fedha ambazo ni malimbikizo ya mafao (accrued liabilities) ya Watumishi wa Umma kabla ya mwezi Julai mwaka 1999. Nakisi ya malimbikizo hayo yanatokana na tathimini iliyofanywa na mthamini (acturial valuer) M/s Genesis Actuarial Solutions kampuni kutoka Afrika Kusini.
Ninapenda kutoa ufafanuzi kuwa taarifa iliyotolewa na vyombo vya habari kuwa kiasi kilichotajwa ni nakisi ya malimbikizo ya mafao ya watumishi na sio hasara ya upotevu wa fedha.

Hata hivyo, katika mwaka wa fedha 2010/2011 Serikali ilikubali kuanza kurejesha mafao yaliyolipwa awali kwa wafanyakazi waliostaafu kazi kuanzia mwaka 2004.

v  Mfuko umekuwa ukitoa mikopo bila ya kutoza riba.
Kuhusiana na taarifa kuwa PSPF imekuwa ikitoa mikopo bila ya kutoza riba siyo sahihi.

Taarifa sahihi ni kwamba kiasi cha fedha kilichoonyeshwa kwenye ripoti ni mikopo (principal amount)  ambayo haikujumuisha riba na siyo kwamba mikopo hiyo haitozwi riba. Mikopo hiyo hutozwa riba na adhabu hutolewa pindi inapocheleweshwa kurejeshwa na wakopaji.

Ni imani yangu kuwa, waandishi wa habari wataendelea kuuhabarisha Umma wa Tanzania juu ya ripoti zangu kwa usahihi na pale patakapokuwa hapaeleweki, naomba mje ofisini kwangu kwa ufafanuzi.



Francis Mwakapalila
K.n.y MDHIBITI NA MKAGUZI MKUU WA HESABU ZA SERIKALI

Wema vs Penny: Marafiki waliogeukana

Wema vs Penny: Marafiki waliogeuka maadui, kisa msanii wa mtoto uswazi Mbagala, Diamond.
Diamond 'aliyetongozwa' na Wema na Penny, sasa aamua kumuanika hadharani Wema aliyemfuta matongotongo ya kupendwa kwa kumrekodi na kuweka hadharani secret yao.
Maisha hubadilika Diamond, ipo siku utamwangukia Wema na kumponda Penny...mapenzi ni kitu kingine, tutashuhudia na kuandika tena na tena...jifunze DIAMOND mambo ya USWAZI achana nayo...!