http://www.mkcomputertweaks.com/mkgroup/fkbmksb.gifMatangazo

Tangaza nasi: mkatedaniel@gmail.com, +255 7666-00 69 70, +255 655-00 69 71, +255 787- 249594

Usilikose kila Jumapili

Jumanne, 16 Aprili 2013

Mtoto wa Rais atiwa nguvuni Senegal kwa utapeli


Karim Wade

Mwanawe rais wa zamani wa Senegal Abdoulaye Wade, ametiwa nguvuni kwa kujipatia dola bilioni 1.4 wakati wa utawala wa baba yake .
Karim Wade ambaye alihudumu katika serikali ya baba yake alikuwa na nyadhifa mbalimbali wakati huo .
Wade aliwasilisha waraka wa orodha ya mali zake katika mahakama maalum ya Senegali iliyopewa jukumu la kuchunguza kesi za ufisadi jana asubuhi.
Alipewa muda wa mwezi mmoja kuthibitisha kuwa alichukua zaidi ya dola bilioni kihalali wakati baba yake alipokuwa madarakani.
Karim Wade alipewa jina la bandia 'Waziri wa Anga na Dunia', alipokuwa waziri wa miundo mbinu, mipango ya miji, usafiri wa anga na ushirikiano wa kimataifa kwa wakati mmoja.
Wakati huo pia alikuwa mkuu wa theluthi moja ya matumizi ya taifa. Mahakama ya Senegali bado haijaeleza sababu ya kumtia rumande na mawakili wa Karim Wade wamesema alichukuliwa kwa nguvu .

source: bbc