Wauguzi watano wameuawa Sudan
Kusini baada ya wanajeshi kushambulia hospitali moja kulipiza kisasi kwa
mauaji ya wanajeshi wengine wanane.
Hii ni kwa mujibu wa mbunge mmoja wa eneo hilo.Viongozi wa kijamii wamethibitisha hospitali hiyo iliyoko katika jimbo la Eastern Equatorial ilishambuliwa ingawa taarifa kutoka ofisi ya gavana wa jimbo hilo imekanusha habari hizo.
Amesema kuwa jeshi lilikwenda pale kulinda raia.
Ufyatulianaji wa risasi kiholea.
Wanajeshi walipelekwa katika eneo hilo, baada ya walinzi wanane wa gavana wa jimbo hilo kuuawa walipotumwa kuwasaka wezi wa mifugo.Mwandishi wa BBC wa masuala ya Sudan Kusini, Nyambura Wambugu anasema wakazi wengi wa eneo hilo lenye milima, wamejihami vikali wakiwa na maguruneti ambayo yalianguka mikononi mwao kufuatia vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miongo miwili.
Mayo alisema kuwa wanajeshi 13 wanapatiwa matibabu mjini Torit.
Lakini amelaumu wanajeshi kwa mashambulizi hayo, akisema kuwa waliwafyatulia risasi watu kiholela walipowasili katika eneo la Lorema, kabla ya kushambulia hospitalini hiyo na kisha kuteketeza makazi ya watu.
Daktari mmoja, mgonjwa mmoja na wauguzi wanne waliuawa.
source: bbc